Mkuu wa mkoa wa shinyanga Dkt Philemon L. Sengati leo tar 14.09.2021 amefanya ziara ya kikazi wilaya ya kishapu, Lengo ni kukagua miradi ya maendeleo baadhi ya maeneo ya wilaya ya kishapu ikiwemo sekondari ya kishapu ambayo ilipewa shilingi 133,200,000/= kwajili ya ujenzi wa mabweni, vyumba 2 vya madarasa na matundu 12 ya choo.
Dkt Sengati baada ya kupokea riport ya ujenzi kutoka kwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi ndg; Mabuguri Mahende Samweli, na kujiridhisha na ukaguzi,amempongeza mkurugenzi mtendaji (w) na viongozi wengine kwa usimamizi mzuri wa fedha za umma kutumika kama ilivyokusudiwa kwenye miradi ya maendeleo ili kuwanufaisha wanafunzi katika masomo yao wasome katika mazingira mazuri na rafiki ili kuwaletea maendeleo katika elimu yao wanayoipata pindi wakiwa shuleni hapo.
“Nawashukuru sana Kishapu kwa ujenzi unaoendelea nimekagua nimeridhika na kasi ya maendeleo ya ujenzi inayoendelea, mabadiliko niliyoyakuta toka nije ziara ya 03.08.2021 ni mabadiliko ambayo yanaridhisha mno, kama tu nilivyosema Kishapu mnaweza sana,na kuweni wabunifu na serikali inayongozwa na Mhe Samia Hassan inataka vitendo zaidi, na mimi sitakubali aibu kwenye mkoa wangu, Mkurugenzi endelea kuhakikisha unasimamia inavyotakiwa miradi hii, ili kuhakikisha fedha za umma zinatumika kama ilivyoelekezwa, nawapongeza sana sana kwa maendeleo haya” pia aliwashukuru viongozi wa chama
“nawashukuru sana viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) Kwa kushirikiana nasi katika kufatilia kwa ukaribu miradi ya maendeleo ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma na kuhakikisha mnatekeleza vyema ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)”
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Lucas Nyanda, amemshukuru sana mkuu wa mkoa Dkt Sengati kwa ziara yake kwenye wilaya ya Kishapu, ameahidi kumpa ushirikiano Dkt Sengati, kuhakikisha kishapu inasonga mbele na inapiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwa sababu Kishapu inaweza na ina watu wachapakazi
“ kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kishapu nakushukuru mkuu wa mkoa kwa ziara yako nzuri katika wilaya yetu, yenye lengo zuri la kutuletea maendeleo katika wilaya yetu, nakuahidi tupo tayali kushirikiana na wewe kuhakikisha kishapu tuna ivusha kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine tumechoka kusikia sehemu zingine wakipongezwa wakati hata sisi uwezo tunao, na bahati nzuri tuna viongozi wengi wachapakazi, niwatu wacheche tu ambao wanakwamisha maendeleo yetu ya kishapu lakini tutashughulika nao.”
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa