Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema ameupongeza uongozi wa mgodi wa madini ya almasi Mwadui Williamson Diamod (WLD) kwa kutia saini mkataba wa hali bora ya wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kuboresha masirahi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo,
Pongezi hizo amezitoa leo wakati akishuhudia utiaji saini mkataba wa hali bora ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ulifanyika katika viwanja vya Mwadui, ambapo amefurahishwa sana na kampuni ya Williamson kwa kuwathamini wafanyakazi na kuweza kuwaboreshea masirahi yao.
Mjema amesema kwa hicho kilichofanyika leo anaitaka na migodi mingine, taasisi mbalimbali ziboreshe masrahi ya wafanyakazi wake ili waweze kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi zaidi na kwa kutimiza matakwa ya wafanyakazi.
,"Bila wafanyakazi kuboreshewa masirahi yao hali ya kufanya kazi inakuwa ni ya kusua sua, lakini akiboreshewa anakuwa na mori ya kuweza kufanya kazi, hivyo tunakushukuru sana meneja wa mgodi huu kwa sababu unamuunga mkono Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu, hivyo na taasisi zote zihakikishe zinawa mikataba wafanyakazi wake,"amesema Mjema.
,"Hakikisheni mnafanya kazi kwa weledi mkubwa na kupendana kwa sababu mmeboreshewa masilahi yenu, pia mhakikishe, mnasainiwa na kamishina wa kazi ili uanze kufanya kazi mara moja, kwani mkataba huu una lengo la kukuza fursa na kuboresha utendaji wa kazi,"amesisitiza Mjema.
Aidha Mjema amewataka wahakikishe wageni wote wanaofika katika kampuni wanakuwa na vibali maalumu vya kufanya kazi kwa kanuni na sheria ya nchi,"amesema mkuu wa mkoa Mjema.
Kwa upande wake meneja mkuu wa mgodi wa WLD mhandisi Ayubu Mwenda amesema ni muda mrefu hawakuwa na mkataba wa namna hiyo kwa sababu ya ugonjwa wa Covid 19, lakini kwa vile alikuwa na malengo ya kuboresha maisha ya wafanyakazi pamoja na kuboresha mahusiano na majirani pamoja na serikali amelitimiza lengo hilo.
"Baada ya kuingia hapa tulikubaliana na wafanyakazi kuwa tutaboresha masirahi ya wafanyakazi, na pia tusisahau kwamba shughuli za uzalishaji zikiongezeka ndio itatuwezesha kuwa na mchango kwenye uchumi wa nchi, mkoa, wilaya na kwenye vijiji vinavyotuzunguka michango itaongezeka zaidi,"amesema.
Naye katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa migodi TAMICO Lukas Bujashi amesema kupitia mkataba wa hali bora tutaenda kuboresha zaidi wanaamini baada ya miaka mitatu mkataba huo utaendelea, hivyo wafanyakazi waliokengeuka wakaenda kusikojulikana warudi kwenye vyama vya wafanyakazi.
,"Sisi tunaamini mkataba huu utaleta ufanisi zaidi kwa wafanyakazi na hamasa kubwa, hivyo tutaweza kumshawishi mwajili tuendelee katika kiwango cha juu, hivyo wafanyakazi waliokengeuka rudini kwenye shina, hivyo leo tamico inashukuru kwa tukio hili tunaheshimu majadiliano, kwani mkataba huu utadumu kwa muda wa miaka mitatu,"amesema Bujashi
Akisoma risala katibu tawi Gatti Raphael amesema anaishukuru kampuni hiyo kwakuthamini wafanyakazi wake, kwani hata baada ya kutokea ugonjwa wa Covid 19 haikupoteza hata mfanyakazi mmoja wameshukuru kwa kuwapatia mkataba hivyo wamesema watafanya kazi kwa weledi na kwa bidii kwa sababu wameboreshewa masirahi yao.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akionyesha keki iliyoandaliwa na wafanyakazi wa mgodi huo
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akilishwa keki na mfanyakazi wa mgodi huo
Mfanyakazi wa mgodi wa WLD akiandaa keki
Mkuu wa mkoa na viongozi wenzake wakiibariki keki kabla ya kukata
Meneja wa mgodi wa WLD akiwa na katibu wa kanda wakisaini mkataba wa wafanyakazi
Mkuu wa mkoa wa Shinysnga Sophia
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akishuhudia wakisaini mkataba wa wafanyakazi wa mgodi ws
Mfanyakazi akimlisha keki meneja wa mgodi wa WLD
Meneja wa mgodi wa WLD na katibu wa kanda TAMICO wakionyesha mikataba hiyo baada ya kusaini
Meneja wa mgodi wa WDL mhandisi Ayubu Mwenda akizungumza
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa