Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe ZainabTelack amesema Serikali inaendelea kusimamia sekta ya kilimo na kuhakikishakuwa kinawakomboa wananchi.
Mhe. Telack ametoa kauli hiyo Agosti 8,2018 katika maonesho ya Kilimo 'Nanenane' yaliyofanyika kitaifa katika viwanjavya Nyakabindi Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
Alisema kuwa Serikali mkoani humo inahakikishaTanzania ya viwanda inawezekana kwani kilimo kitasaidia viwanda kupata malighafiza kuzalisha bidhaa mbalimbali hususan za zao la pamba.
"Bila kilimo hatuendi popote nasisi tunamuunga mkono Mheshimwa Rais kwa kusimamia kilimo kwa nguvu zotenakuhakikisha kilimo kinamkomboa mwananchi," alisema.
Mkuu huyo wa mkoa aliongeza kuwaShinyanga ina viwanda zaidi ya 40 ambavyo vinafanya kazi ya kuongeza thamani yazao la mpunga kutoka mashambani.
Aidha, Mhe. Telack aliongeza kuwa mkoahuo unajitosheleza kwa chakula kutokana na wananchi kuitikia wito wa kutekelezadhana ya kilimo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa