Shirika la Relief for Development Society (REDESO) leo April 15, 2020 limefanya ziara kukagua miradi ya maendeleo kwa wanavikundi katika wilaya ya kishapu mkoani Shinyanga.
Miradi hio inayowezeshwa na REDESO ni pamoja na shamba la viazi lishe aina ya Jewel lenye ukubwa wa nusu heka linalomilikiwa na kikundi cha akina Mama 14 katika kijiji cha Inolelo kata ya Ngofila. Mradi wa kifaa cha kukaushia mazao. Mradi wa zizi la ng’ombe kwa ajili ya kunenepesha ng’ombe katika kijiji cha Ngofila kata ya Ngofila unaomilikiwa na kikundi cha Hapa Kazi tu. Mradi wa banda kwa ajili ya kufuga nguruwe wa kikundi cha Umoja wa Vijana katika kijiji cha Kiloleli kata ya Kiloleli. Mradi wa zao la pamba na mtama unaomilikiwa na kikundi cha Kalangali kijiji cha Kiloleli kata ya Kiloleli.
Lengo la miradi hii ni kutumika kama darasa kwa wanavikundi, pia kutumika kama chanzo cha kipato na kujikwamua kiuchumi kwa familia zao. Akitoa ufafanuzi juu ya miradi hii, Afisa Miradi katika Shirika la REDESO, Vera Cleophas amesema kutokana na mwitikio wa wanajamii REDESO inawawezesha na kuinua familia katika Nyanja mbalimbali ili kujikwamua kwenye umasikini .
“katika wilaya ya Kishapu tumeanzisha miradi ambayo itatumika katika kutatua changamoto za kiuchumi ka wanufaika na jamii kwa ujumla. Hivyo wana vikundi wanapaswa kutumia fursa hizi ili kuinua familia zao kiuchumi”
Katika msimu huu wa kilimo, wanavikundi wametumia fursa hii kulima kilimo cha pamba na mtama na kufuga mifugo kama ng’ombe na nguruwe kwa ajili ya biashara ambayo itatumika katika kukidhi mahitaji yao na familia zao.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa