Serikali mkoani Shinyanga imeahidi kutatua changamoto zinazowakabili watumishi pamoja na kuendelea kuwatetea ili kuhakikisha wanafanya kazi wakiwa katika hali ya usalama.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack wakati akizungumza katika sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) kimkoa zilizoadhimishwa kimkoa wilayani Kishapu
Alisema kuwa wapo watumishi wanaocheleweshwa kupandishwa vyeo kutokana na sababu mbalimbali hivyo Serikali ya Mkoa itahakikisha watumishi wanapata stahili zao kwa wakati.
Kwa upande mwingine Mhe. Telack ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo alisema Serikali pia itahakikisha wafanyakazi wanaostaafu wanapata pensheni zao kwa wakati.
Aliwataka kukujituma na kuwajibika katika maeneo yao ya kazi na kuwa Serikali ipo pamoja na watumishi na kuwa kuwajibika kwao kutawezesha kuinua uchumi na kuleta maendeleo.
Aidha Mhe. Telack aliwataka watumishi kutumia fursa mbalimbali zilizopo nchini ili kujipatia kipato cha ziada ili kufanikisha falsafa ya uchumi wa viwanda inayotekelezwa hapa nchini.
Aliwapongeza waanyakazi wote kwa kujituma katika maeneo yao ya kazi na kuwataka viongozi wao wawaelekeze vizuri kanuni na sheri za kazi badala ya kuwabeza.
"Tunatambua wafanyakazi wapya wanapotola masomoni wanakwa hawajafahamu vizuri taratibu za kazi hivyo ninyi viongozi mnapaswa kuwapa maelekekezo kuhusu sheria za kazi na pia kuwaonya wanapokosea" alisisitiza.
Pia Mkuu wa Mkoa aliwataka viongozi wa vyama vyote vya wafanyakazi kukaa pamoja na kujenga uhusiano na wanachama wao ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea.
Sherehe za Meo Mosi mwaka huu zilikuwa na kaulimbiu isemayo 'Kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii kulenge kuboresha mafao ya wafanyakazi' ambao kitaifa zilifanyika mkoani Iringa mgeni akiwa Rais Dkt. John Magufuli.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa