Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia imetoa jumla ya vitabu 29,821 vya kujifunzia na kufundishia kwa shule za msingi katika Halmashauriya Wilaya ya Kishapu kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu.
Vitabu hivyo vilivyopokelewa leo Septemba 7, 20118 vimetolewaikiwa ni sehemu ya mpango wa elimu bila malipo ambao unaendelea kutekelezwa katikashule za msingi na sekondari nchini kote.
Akizungumza wakati wa zoezi la kupokea vitabuhivyo, Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Sostenes Mbiwlo aliishukuruSerikali kwa msaada huo na kusema vitachangia kuboresha sekta hiyo.
Alisema kuwa vitabu vimeanza kusambazwa katikashule za msingi wilayani humo ambapo vitatumika kwa wanafunzi kujifunzia navingine vitakuwa ni vitabu vya mwongozo kwa walimu.
Mbwilo alivitaja vitabu hivyo kuwa ni vya masomo yaHisabati, Kusoma kwa ajili ya kufundishia madarasa ya kwanza na ya tatu pamojana Kuhesabu kwa ajili ya kufundishia darasa la pili.
Vitabu vingine vilivyopokelewa ni Kiswahili, Uraiana Maadili kwa ajili ya kufundishia darasa la tatu na nne na Sayansi darasa lanne.
Aidha, Afisa Elimu huyo alisema kuwa Halmashauriimepokea vitabu vya kiongozi kwa walimu kwa ajili ya masomo ya Kingereza,Kiswahili, Hisabati, Sayansi na Maarifa ya Jamii.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa