Shirika lisilo la kiserikali linaloitwa ANNA SCHUBERT MACKEJA KUOJIE Foundation ASMK limetoa msaada wa Saruji na Magudulia 140 katika Shule ya Busiya Wilayani Kishapu yatakayotumiwa na wanafunzi kwa ajili ya kufuata na kuhifadhi maji
Shirika hilo limetoa magudulia hayo kwa lengo la kuwaondolea usumbufu wanafunzi kutoka na ndoo nyumbani kwa ajili ya kufuata maji kwenye vyanzo vinavyopatikana umbali mrefu kutoka katika eneo la shule.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo, Mratibu wa utemi wa Busiya Mzee Alfred Muyanga amesisitiza Walimu na wanafunzi kuyatunza magudulia hayo ambayo yatasaidia kuhifadhi maji hivyo kutoa fursa kwa wanafunzi kuhudhuria vipindi darasani.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Busiya Mwalimu Badi Iddi Mfinanda amepongeza na kusema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto zilizopo.
Nao baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Busiya wamelishukuru shirika la ASMK kwa kutoa msaada huo ambao utasaidia kupunguza changamoto zao.
Aidha afisa mtendaji wa kata ya Itilima akizungumza kwa niamba ya afisa elimu wa Halmasuri ya Wilaya ya Shinyanga, Renatus Malima amelipongeza na kulishukuru shirika la ASMK kwa kutuoa msada wa magudulia 140 na saruji katika shule ya sekondari Busiya ambapo amewaomba kuendelea na majitoleo hayo kwa lengo la kuisaidia serikali kutatua changamoto zilizopo.
ANNA SCHUBERT MACKEJA KUOJIE ASMK ni shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta za elimu na maji Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga,ambalo lipo chini ya himaya ya utemi wa Busiya wa Mtemi Edward kidaha Makwaiya.
Mbele upande wa kulia ni mratibu msaidizi wa utimi wa Busiya Bwana Nicholaus Luhende na upande wake wa kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Busiya ambapo nyuma ni viongozi wa shirika la ASMK wakitembelea mazingira ya shule hiyo.
Viongozi wa shirika la ASMK wakipewa kitabu cha kusaini wageni.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa