Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imefanya zoezi la kutoa chanjo ya minyoo na kuogesha mifugo ya walengwa.
Zoezi hilo lilifanyika kwa walengwa wa kaya katika vijiji vya Masagala, Mwadui Lohumbo na Mpumbulu kwa kushirikiana na maafisa Mifugo wa kata ambapo liliambatana na utoaji elimu.
Mratibu wa TASAF wilayani humo, Sospeter Nyamhanga akiambatana na mhasibu Rahman Selemani alisema zoezi hilo linafanywa ili kuwatia hamasa walengwa kuwa na utamaduni wa kupa kinga mifugo yao.
Alisema lengo la mpango huo ni kuwakwamua walengwa kiuchumi na hivyo kwa kutumia ruzuku wanayopata mbali na kupata huduma mbalimbali pia wananunua mifugo ikiwemo mbuzi, kondoo, kuku na bata.
“Tunashukuru zoezi hili linakwenda vizuri na kama unavyoona hapa wanakuja walengwa na mifugo yao kasha wataalamu wetu wanaipatia chanjo ya minyoo na kuiogesha hivyo kuhakikisha haipati magonjwa,” alisema Nyamhanga.
Aidha, mratibu huo aliwataka walengwa wengine kuhamasiska na kununua mifugo kama walivyofanya wenzao jambo ambalo litawaondoa katika umaskini kwani wataweza kuuza mifugo hiyo au mazao yake.
TASAF imekuwa ikiwezesha kaya maskini kwa kutoa ruzuku kila baada ya miezi miwili ambayo huwawezesha kuwapatia huduma mbalimbali zikiwemo za afya na elimu.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa