Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kupitia Mfuko waMaendeleo ya Jamii (TASAF) imetoa sh. milioni 242.8 kwa ajili ya kuwezesha kayamaskini katika kipindi cha mwezi Julai hadi Agosti, 2018.
Mratibu wa TASAF wilayani humo, Sospeter Nyamhangaamebainisha hayo jana ambapo amesema fedha hizo zimetolewa kuwezesha jumla yakaya 5923 katika vijiji 78.
Alisema zoezi hilo limeendelea kupata mafanikiokutokana na walengwa wengi kufanyia kazi elimu wanayopatiwa na wataalamu kuhusumatumizi sahihi ya fedha wanazowezeshwa.
Nyamhanga aliongeza kuwa kutokana na ufuatiliaji wamara kwa mara unaofanywa baadhi ya kata zimeonesha mabadiliko ya kimaisha kwakutumia ruzuku wanazopata kufanya shughuli zinazowapatia kipato.
“Tumetembea kaya mbalimbali huko vijijini nakiukweli tumekuta walengwa wa Mpango wa TASAF wanafuga mifugo kama kuku, kondoona mbuzi na wengine wameanzisha biashara ndogndogo na hilo ndilo lengo letuhasa,” alisema.
Aidha, alibainanisha TASAF pia imewawezeshawananchi kuboresha makazi yao kutoka nyumba za tembe na nyasi na kujenga nyumbaza tofali na bati.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa