Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Ndg; Emmanuel Johnson
Leo Tarehe 20.04.2022 Amefungua Mafunzo ya Siku 6 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, kwa wawezeshaji wa mamlaka za maeneo Utekelezaji kuhusu maandalizi, Utekelezaji na Usimamizi wa Miradi ya kutoa Ajira za Muda chini ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) Awamu ya Tatu kipindi cha pili.
Katika awamu ya Tatu kipindi cha pili inaendelea kutekeleza jumla ya Miradi ya Ajira za Muda 3185 katika Mamlaka ya Maeneo ya Utekelezaji 51 kwa Mwaka 2021/2022.Katika kipindi cha 2022/2023 jumla ya Mamlaka za maeneo ya Utekelezaji 123 zitatekeleza Miradi ya kutoa Ajira za muda ikiwa ni ongezeko la Mamlaka za maeneo ya Utekelezaji 72.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa