Kamati ya maafa ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na Relief for Development Societies (REDESO) imefanya tathimini leo tarehe 28/04/2020 juu ya hali ya ugonjwa wa Corona wilayani Kishapu.
Kamati hio inayoongozwa na mwenyekiti wa kamati ya maafa ya wilaya, Sostenes Mbwilo iliunda kamati ya uratibu yenye wajumbe wa CMT, Taasisi mbalimbali na kamati ya ulinzi na usalama. Kamati nyingine ndogondogo zilizoundwa ni kama vile kamati ya logistic na ugavi inayohusisha manunuzi na ugawaji wa vifaa mbalimbali, kamati ya Ufuatiliaji inayohusu kufuatilia matukio yote zinazotokea katika wilaya pia kutoa ushauri wa uvaaji wa barakoa na kunawa mikono, kamati ya wash inayohusu kunawisha watu mikono katika minada ya Mhunze, ukenyenge, Maganzo, Magalata, Seke Ididi pia uhamasishaji kwa wafanya biashara kuwa na vifaa vya usafi katika maeneo yao ya kazi, kamati ya maabara kwa ajili ya kuchukua sampuli kwa wagonjwa, kamati ya psychosocial support kwa ajili ya masuala ya saikolojia, kamati ya mazishi kwa ajili ya masuala ya mazishi.
Pia watendaji wa vijiji, watendaji wa kata na maafisa tarafa wameshauriwa kutoa taarifa wanapotokea wageni katika maeneo yao. Pia katika nyumba za wageni wanafatiliwa kujua mama kuna mtu mwenye dalili za ugonjwa wa corona. Pia kwa kushirikiana na watu wa Redcross wamefanya matangazo vijijini kuhusu elimu juu ya corona. Pia mafunzo kwa watumishi wa Afya na halmashauri.
Katika kikao hicho ilibainika kuwa katika kituo cha afya Kishapu ambacho ndio kilichoteuliwa kama kituo cha wagonjwa wa corona kuwa na uhaba wa dawa kama vidonge vya chlorine kwa ajili ya usafi na vifaa vya kutosha kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa, kama N95 kwa watoa huduma.
Kwa upande wa mafanikio tumefanikiwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii na mwitikio ni mkubwa ambapo hadi sasa katika wilaya ya Kishapu hakuna mgonjwa wa corona.
Mapendekezo yalitoyolewa na kamati ni kama vile, kuwekwe kituo maalumu kwa ajili ya kushusha abiria wanaotoka maeneo mbalimbali kuingia wilayani Kishapu kama vile stendi kubwa ya Mhunze na kuorodhesha majina ya kila abiria ndani ya gari ili kurahisisha ufuatiliaji pia kunawa mikono. Idara ya kilimo ilipendekeza kuwa jamii ielimishwe juu ya kuhifadhi chakula pia kuwa na matumizi mazuri ya chakula kwa ajili ya baadae. Kuanzia mwezi Mei kutakuwa na msimu wa Pamba hivyo Chama cha Ushirika AMCOS kiandae vifaa vya kujikinga na corona kama vile vifaa vya kunawa mikono. Kwa upande wa Afya kuendelea kuomba dawa na vifaa kinga pia kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya kujikinda na ugonjwa wa corona.
Katika kikao hicho REDESO kama mdau wa kukabiliana na majanga kama vile ya kuipinga corona iliahidi kutoa msaada wa ndoo kwa ajili ya kunawa mokono katika katika vijiji thelathini ambavyo vina miradi yao. Katika vijiji hivyo zitatolewa ndoo kwa ajili ya zahanati zilizoteuliwa kwa ajili ya wagonjwa wa corona. Pia katika ofisi za vijiji kutawekwa ndoo kwa ajili ya kunawa mikono, pia kwa makundi maalumu kama wathirika wa UKIMWI watapatiwa huduma ya kunawa mikono na sanitizers katika maeneo yao ya kutolea huduma.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa