Halmashauri ya wilaya Ya Kishapu mkoani Shinyanga chini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeboresha daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili kwa mwaka 2020. Zoezi hili limefanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 17/04/2020 hadi tarehe 19/04/2020 katika vituo 29 ambapo kila kata ilkuwa na kituo kimoja.
Katika kuboresha taarifa za wapiga kura, kulikuwa na marekebisho kama vile majina ya watu, miaka ya kuzaliwa, kuondoa taariza za vifo, pia kuandikisha wapiga kura wapya waliofikisha umri wa miaka 18 na wale ambao wataifkisha miaka 18 ifikapo tarehe 24 mwezi Oktoba mwaka 2020, kuhamisha taarifa za wapiga kura kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine.
Akitoa takwimu juu ya zoezi la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili kwa mwaka 2020, Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya W kilaya ya Kishapu, Sigisbert Rwezaula amasema zoezi lilienda vizuri kwa sababu wananchi walikupewa taarifa juu ya zoezi hili na kubandikwa majina yao kwenye kila kituo.
“waliojiandikisha wapya katika daftari la kudumu la wapiga kura walikuwa 1872, walioboresha taarifa zao walikuwa 1879 na waliotolewa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura walikuwa 24, hivyo jumla ya watu waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa awamu ya pili walikuwa 3771”
Katika zoezi la kuboresha taarifa za wapiga kura kulikuwa na changamoto kama vile, upungufu wa fomu namba 5A ambayo ilkuwa inahusu kuboresha taarifa za mpiga kura, lakini Afisa uchaguzi aliwasiliana na tume ya uchaguzi na fomu hizo ziliwasili tarehe 18/04/2020, pia miundombinu ziliharibika kutokana na mvua kunyesha kwa muda mrefu.
Afisa Mwandikishaji pamoja na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wanaishukuruTume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na timu nzima ya Uboreshaji wa daftari la kudumu la Mpiga kura awamu ya pili kwa mwaka 2020 kwa ushirikiano waliouonyesha katika zoezi hili.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa