Utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu umezidi kushika kasi ambapo ujenzi wa miundombinu ya elimu umepiga hatua katika shule za msingi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Stephen Magoiga na timu ya wataalamu kutoka wilayani humo wametembelea miradi hiyo ya elimu inayoendelea kutekelezwa katika sekta hiyo nyeti.
Katika ziara hiyo wamejionea maendeleo ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na nyumba za walimu katika shule ya msingi Migunga kata ya Mwataga ambazo ni fedha zinazotolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Tayari vyumba vya madarasa vimeshaezeskwa huku ujenzi wa vitu vingine ukiendelea wakati ujenzi wa nyumba za walimu umeshaanza kupitia fedha hizo hizo kama ambavyo Halmashauri inatekeleza mpango wake wa 2017/2018.
Miradi hiyo pamoja na kutekeleza na Serikali lakini pia nguvu za wananchi zinashirikishwa ili kuhakikisha inafanikiwa kwa kiwango kikubwa na hivyo kuwa msaada kwa jamii.
Hivi karibuni TEA ilitoa jumla ya jumla ya sh. milioni 321 kwa Kishapu kwa ajili ya kufanikisha ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu ya shule za msingi wilayani humo.
Miongoni mwa shule zinazonufaika na mpango huo ni pamoja na Migunga ambayo imetengewa sh. milioni 60 kwa ajili ya vyumba vitatu vya madarasa ambapo kati hizo sh. milioni 30 zimepokelewa.
Halmashauri ya Kishapu pamoja na kupokea fedha imekuwa ikitumia ubunifu kufanya kitu cha ziada ambapo imeweza kujenga chumba cha ziada cha darasa sanjari na nyumba ya walimu.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa