Afisa usafirishaji Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Ndg; Mathias Likenejo amefanya ukaguzi wa pikipiki za serikali kwa kushirikiana na fundi mkuu wa wilaya Ndg; Paul Maganga, ukaguzi huo umefanyika kwa siku mbili katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu na kubaini baadhi ya pikipiki kuwa mbovu na zingine zinazohitaji matengenezo ya kawaida.
Paul Maganga, Fundi mkuu wa wilaya baada ya ukaguzi wa pikipiki za serikali amebaini pikipiki nyingi ni mbovu zinahitaji matengenezo makubwa na baadhi ya pikipiki ambazo zinahitaji matengenezo ya kawaida,
“Tumefanya ukaguzi wa pikipiki za serikali, obaada ya ukaguzi tumebaini pikipiki nyingi ni mbovu na zinahitaji matengenezo , na hii ni sababu ya watumishi kutokujijengea tabia ya kufanya service mara kwa mara, hivyo kupelekea pikipiki kuwa na matatizo makubwa, niwaombe basi ambao hawajaleta pikipiki kukaguliwa wazilete zifanyiwe ukaguzi”
Mathias Likenejo, Afisa usafirishaji Halmashauri ya wilaya ya Kishapu,amesema lengo kubwa la ukaguzi ni kutaka kujua pikipiki walizo kabidhi kwa watumishi zipo zote, na zinatunzwa kama inavyotakiwa,
“Kwanza kabisa lengo la kukagua pikipiki nikutaka kujiridhisha pikipiki hizi zipo zote na zinafanya kazi? Maana kuna watumishi wengine wamehama unaweza kukuta Kahama na pikipiki yetu, Jambo la pili ni kubaini watu walioshindwa kufanya marekebisho ili tuwasaidie kutunza, na maanisha tutawanyang’anya na tutawakabidhi wengine ambao wataweza kuzitunza"
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa