Zoezi la uwekaji wazi Daftari la kudumu la Wapiga Kura Awamu ya pili katika Wilaya ya Kishapu imeanza rasmi leo tarehe 17 June 2020 hadi tarehe 20 June 2020 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni katika eneo la Mhunze Stooni.
Afisa Uchaguzi Wilaya ya Kishapu Sigisbert Rwezaula amesema zoezi hili la uwekaji wazi daftari la kudumu la wapiga kura ni kwa ajili ya marekebisho ya taarifa za wapiga kura katika vituo vyote vitivyotumika katika zoezi la awali hivyo wananchi wanatakiwa kwenda katika vituo hivyo kuhakiki taarifa zao mapema.
Katika zoezi hili, taarifa ambazo zitahakikiwa ni kama vilejina, jinsi, tarehe na hakutakuwa na uhamisho wa taarifa za mpiga kura kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine.
Aidha, Afisa Uchaguzi ametoa rai kwa wananchi wote wafike kwenye vituo walivyojiandikishia kuhakiki taarifa zao na iwapo kutakuwa na marekebisho yoyote wasisite kufika katika kituo cha Mhunze Stooni kwa ajili ya kufanya marekeshisho ya taarifa zao.
Aidha, katika zoezi hili la uwekaji wazi daftari la kudumu la wapiga kura, ofisi ya Mkurugenzi inapenda kuwakumbusha wananchi kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona kwa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni ya maji.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa