Wananchi wa wilaya ya Kishapu wameipongeza sana TANROADS kwa kuwakumbuka kuwafungia taa zinazo tumia mionzi ya juu kwenye barabara kuu inayo tokea shinyanga manispaa richa tu ya ulinzi lakini pia zinapendezesha mji na kuonekana wa kitofauti kidogo na kule muonekano tofauti
Baadhi ya wanachi walipata nafasi ya kuzungumza kuhusu furaha waliyo nayo, kipindi wakizungumza na afisa habari wilaya ya kishapu wakiwa na furaha kubwa kabisa katika kueleza ya moyoni
Kija Dutu mfanyabiashara Kishapu, ametoa shukurani za dhati kwa TANROADS kwa kuwakumbuka wilaya ya kishapu kwani ni mji ambao unakuwa kwa haraka na unarahisisha uendeshaji washughuli pamoja na urahi wa watumiaji wa barabara kupukana na ajali kipindi cha usiku hasa maeneo yanayokuwa na watu wengi kama katikati ya senta
“Nitoe shukurani zangu za dhati kwa TANROADS kwa kutufungia taa hizi za solar kwani ni muhimu sana kwa miji ambayo inaendelea kukua kama Kishapu, itawarahisishia watumiaji wa barabara kuepukana na ajali kwa urahisi, hasa sehemu ambazo zinakuwa na watu wengi hata, sisi wafanya biashara inakuwa nzuri kwetu sisi tunaotoa bidhaa nje, kama petrol vinaonekana kwa urahisi kwa mteja natamani barabara zote za mhunze waziwekee hizo taa ili na mji uzidi kunoga bwanaa si unaona unavyopendeza “
Juma Mussa pia ameipongeza TANROADS kwa kuweka taa za mionzi ya jua kwa sabaubu zinaimarisha ulinzi na usalama wa raia wanaotumia barabara hiyo ni rahjisi kwa dreva na raia kuepuka ajali kutokana na mwanga wa taa hizo
“kwa kweli kitu kinacho stahili kupewa pongezi kipewe tu mtu akifanya vizuri apongezwe akifanya vibaya akosolewe, pia kwa hili la taa TANROADS wamefanya jambo la maana nililokuwa nikilitarajia siku zote kwanza taa zinasaidia kupunguza ajali, sehemu ambazo zilikuwa za wasisi maana ya giza la kutisha kwa sasa ni rahisi mida ya usiku kupitika , lakina pia niwaombe TANROADS kuhakikisha angalau barabara zote wanawekea taa ili wazidi kuimarisha usalama wa raia”
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa