Jumla ya watahiniwa 1,381 wameanza kufanya mtihani wa Taifa wa kumalizia kidato cha nne katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Afisa Elimu Sekondari Wilaya, Paul Kasanda amebainisha kuwa miongoni mwa watahiniwa hao 89 kati yao ni watahaniwa binafsi (Private Candidates) na 1,292 wa shule mbalimbali.
Aidha, Kasanda amesema Kishapu ina jumla ya shule za sekondari 28 ambapo mbili kati yake zinamilikiwa na watu binafsi na 26 zikiwa chini ya umiliki wa Serikali.
Alisema kuwa zoezi hilo la mtihani wa kumalizia elimu ya sekondari linalofanyika nchi nzima linaendelea vizuri katika vituo vya kata zote wilayani humo.
Wanafunzi hao wa kidato cha nne walioanza Oktoba 30 wanatarajia kumaliza mtihani huo ifikapo Novemba 14 mwaka huu.
Wakati huo Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mh. Nyabaganga Taraba na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga wanawatakiwa watahiniwa wote kila la heri katika mtihani wao.
Pia wamewaomba wawe watulivu wakati wote pamoja na kufuata kanuni zote za mitihani na hatimaye wafanye vizuri.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa