Watahiniwa 222 wanatarajiwa kufanya mtihani waTaifa wa kidato cha sita katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoaniShinyanga.
Akizungumza na ofisini kwake Afisa Elimu Sekondariwa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Paul Kasanda alisema kuwa miongoni mwawatahiniwa hao 219 ni wa kiume na watatu ni wa kike.
Kasanda alizitaja shule zinazotarajiwa kufanyamitihani hiyo ni pamoja na Sekondari Kishapu, Sekondari Shinyanga ambazo zoteni za wavulana na Sekondari ya Mwadui.
Afisa Elimu huyo aliwataka watahiniwa hao kufanyamitihani yao kwa utulivu bila kuwa na hofu ili waweze kufanya vizuri nahatimaye kuingia elimu ya juu.
“Nina imani kuwa wanafunzi wetu watafanya vizurikatika mitihani yao na wote naamini wataingia chuo kikuu, wanafunzihawatatuangusha wilaya yetu,” alisema.
Alisema kuwa anaamini wanafunzi watafanya vizurikwa kuwa wameandaliwa vizuri na walimu wao na wao wamefanya mazoezi ya kutosha.
Mtihani wa Taifa wa kidato cha sita umeanzaJumatatu Mei 7, 2018 na unahusisha shule mbalimbali za sekondari nchini kote zikwemoza Serikali na za binafsi.
Pia pamoja na kuwa na watahiniwa kutoka shulembalimbali pia watahiniwa binafsi (private candidates) pia wanatarajiwa kufanyamtihani huo katika vituo vyao.
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu inawatakiwawanafunzi mtihani mwema na Mungu awasaidie ili waweze kufanya vizuri nahatimaye watimize ndoto yao ya kufika mbali kielimu,
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa