Watahiniwa 4,592 wanatarajiwa kufanya mtihani wakumaliza elimu ya msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambao unafanyikanchini kote Septemba 5 na 6, 2018.
Hayo yamesemwa leo na Ofisa Elimu ya Msingi waHalmashauri ya Wilaya hiyo, Sostnes Mbwilo wakati akizungumza ofisini kwakekuhusu kuanza kufanyika kwa mtihani huo.
Mbwilo ambaye pia ni katibu wa Kamati ya MitihaniWilaya alibainisha kuwa jumla ya shule za msingi 117 zilizopo wilayani humo zimepangwakushiriki katika mtihani huo zikihusisha mikondo 220.
Akizungumzia kuhusu maandalizi alisema kuwayamekwenda vizuri na kuwa vituo vya kufanyia mitihani hiyo kwenye vijijimbalimbali vipo tayari.
“Sisi kama Idara ya Elimu tunaamini tumewaandaavizuri wanafunzi na wamepata mafunzo kutoka kwa walimu wao hivyo tunatarajiakuwa watafanya vizuri mitihani yao,” alisema Mbwilo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji waHalmashauri ya Wilaya ya Kishapu, George Kessy aliwataka wanafunziwanaotarajiwa kufanya mitihani hiyo kuwa watulivu na kujibu maswaliinavyopaswa.
Aliongeza kwa kubainisha kuwa mitihani hiyo nisehemu ya kuwapima uelewa wantahiniwa hao katika kipindi cha miaka sabawaliyokuwa shuleni na watakaofaulu watajiunga na kidato cha kwanza.
Kessy ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati yaMitihani Wilaya aliwataka kutokuwa na hofu na hivyo wanapokuwa kwenye vyumbavya mitihani wayapitie na kuyasoma vizuri maswali na kuyajibu inavyotakiwa.
Mitihani ya darasa la saba kitaifa inahusishamasomo mbalimbali yakiwemo ya Hisabati, Kiswahili, Kingereza, Maarifa ya Jamiina Sayansi ambayo inatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfulululizo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mtendaji wa Barazala Mitihani la Taifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wake, Dkt. Charles Msonde nikuwa jumla ya watahiniwa 960,202 wamesajiliwa.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa