Na Ofisi ya Habari,Kishapu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kuzingatia sheria za kazi.
Magoiga alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akitoa mafunzo kwa watumishi hao kuhusu matumizi ya fedha za ruzuku ya maendeleo inayotolewa kwa mamlaka za Serikali zaMitaa.
Alisema kuwa watumishi wanao wajibu mkubwa wa kufuata utaratibu katika utendaji wao ili kuitangaza vizuri halmashauri hiyo.Aliwataka watumishi kila mmoja kusimamia mradi wa maendeleo katika eneo lake ili kuwapatia wananchi wa Kishapu huduma bora.
"Mambo ni mengi mazuri yanayofanyika katika halmashauri yetu hivyo muwe na moyo wa ushindani na kuyatangaza, kila mmoja atawajibika kutoa taarifa kuhusu mradi wake," alisema Magoiga.Mkurugenzi aliongeza kwa kusema kuwa pamoja na hayo pia wananchi wanawajibika kushiriki katika shughuli za maendeleo badala ya kuiachia Serikali.
Aliwataka madiwani kuhamasisha wananchi wako katika miradi hiyo na kuwa wananchi wanavyoshiriki ndivyo Serikalio inavyoleta maendeleo kwa haraka.
Pia Magoiga alisisitiza kuwepo kwa uwazi katika matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa kwa Serikali za Mitaa.
Aliwataka watendaji hao wa Serikali kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa kufanya tathmini ili kubaini kama kweli miradi hiyo ina tija kwa wananchi.
"Lazima tufanye evaluation (tathmini) baada ya kumalizika kwa miradi ya maendeleo lakini pia wakati miradi inaendelea pia lazima tufanye monitoring kwa ila hatua ya miradi hiyo kama inatekelezwa inavyostahili," alisisitiza.Aidha, mkurugenzi alihimiza ushirikiano baona ya idara na idara na vitengo katika utekelezaji wa miradi ili kuhakikisha uboreshaji wa halmashuri.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa