Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude amewataka watumishi wa Wilaya ya Kishapu kufuata miongonzo Taratibu na Kanuni katika utekelezaji wa Majukumu yao
Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo Tarehe 17, Octoba 2023 alipokuwa anazungumza na Watumishi katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
"Watumishi wote tusimamie Misingi ya Kazi, kanuni za Utumishi zinaeleweka ikiwa ni pamoja na kuwahi kazini, turudini kwenye Misingi yaani tuisimamie ifanye kazi Misingi hii isipofanya kazi tunaiuwa wenyewe kwa hiyo tusimamie misingi hii na Kanuni na tukumbushane Mara kwa Mara na kutekeleza maelekezo ya Viongozi wa Serikali"
Naye Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Bi. Fatma H. Mohammed amewakumbusha Watumishi kuwa na nidhamu kazini na nje ya kazi kwaani wamebeba dhamana kubwa katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Ndugu. Emmanuel Johnson aliwasisitiza Wakuu wa Idara na Vitengo kufanya vikao vya Mara kwa Mara ili kuweza kutambuana na kuweza kushirikiana kwa urahisi katika majukumu.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewakumbusha watumishi kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ndiye Msimamizi Mkuu wa Watumishi wote ndani ya Wilaya.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa