Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wamewafukuza kazi watumishi watatu kwa Makosa ya Utolo kazini
Maamzi ya kuwafukuza kazi watumishi hao yaliazimiwa na Madiwani Tarehe 02 Novemba 2022 kwenye Baraza la Madiwani pindi walipojigeuza kuwa kamati
Akitaja majina hayo mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya watumishi waliofukuzwa kazi ni Alex V Kapula (Daktari Mkuu Msaidizi), Hafidhi Hassan (Msaidizi wa Afya), na Neema C. Nyanda (Maendeleo ya jamii).
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu amewataka watumishi wa umma kuwa waadilifu na wafate kanuni na taratibu za Utumishi wa umma.
Madiwani wakiwa kwenye Baraza
Mkurugenzi mtendaji akizungumza
(Kushoto) Mwenyekiti (kulia) Mkurugenzi
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa