• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Machapisho
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022

WAZIRI BASHUNGWA AWATAKA MA-RC, MA-DC KUSIMAMIA HUDUMA ZA AFYA

Posted on: May 19th, 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchi nzima kusimamia kikamilifu utoaji wa huduma ya dharura katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa kuondoa urasimu unaochelewesha mgojwa kupata huduma.


Bashungwa ametoa maelekezo hayo Mkoani Tabora katika warsha ya Sema na Mama wakati akijibu hoja na kero ya ucheleweshwaji wa huduma kwa wagojwa katika vituo vya kutolea huduma mkoani hapo.


“Utoaji wa huduma za dharura katika vituo vya kutolea huduma za afya itolewe kwa haraka, unaweza kumuhudumia mgojwa wakati utaratibu wa kujaza taarifa na maelezo unaendelea ili kuokoa maisha yake, hivyo nawaelekeza Wakuu wa Mikoa na wilaya kusimamia utoaji wa huduma hiyo katika maeneo yao” amesema Bashungwa


Aidha, Bashungwa amesema Serikali inatambua Machinga kuwa ni sekta rasmi ndio maana imeelekeza kuwapanga katika maeneo rafiki na kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya biashara ambapo itakuwa rahisi kuwafikia na kuwapelekea huduma mbalimbali.


Amesema tayari Serikali imewaelekeza Wakuu wa Mikoa yote kushirikiana na viongozi wa Wafanyabishara wadogo kujadili na kutafuta namna bora ya kuwapanga kulingana na mazingira ya Mkoa husika yatakayowaezesha wateja wao kuwafikia.


Vile vile, Bashungwa amesema Serikali ya awamu ya sita imetoa nafasi ya upekee kwa watu wenye ulemavu katika sekta mbalimbali kama utoaji wa mikopo na ajira ambapo asilimi 3 ya nafasi za ajira zinazotolewa zimeelekezwa kwa watu wenye ulemavu.


Pia, amesema Serikali itaendelea kusimamia utoaji wa Mikopo ya asilimia 10 za halmashauri kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na sasa Wakurugezi watapimwa kwa namna wanavyotenga fedha hizo kwa mujibu wa sheria na utaratibu wa kuzigawa bila upendeleo kwa kuwanufaisha wahusika.


Warsha ya  Sema na Mama iliwakutanisha viongozi wa Serikali na makundi mbalimbali ya wananchi wa mkoa wa Tabora ambao ni Machinga, Wakulima, Boda boda na watu wenye mahitaji maalum na kupata nafasi ya kusikilizwa na kujibiwa moja kwa moja na viongozi hao.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • RATIBA YA UFANYAJI MAZOEZI KWA KILA WIKI August 16, 2021
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ATOA UFAFANUZI KUPANDA KWA BIDHAA

    June 14, 2022
  • BARRICK YA UNGA MKONO UTAMADUNI MKOA WA SHINYANGA

    June 08, 2022
  • TAMASHA LA UTAMADUNI MKOANI SHINYANGA LA ZINDULIWA NA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII.

    June 06, 2022
  • OR-TAMISEMI IMETOA MWONGOZO KWA KIDATO CHA 5 KUBADILISHA SHULE, TAHASUS

    June 06, 2022
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa