Leo Octoba 27.2021 kamati ya utawala, fedha na mipango ikiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri mhe, William Luhende Jijimya imefanya ziara ya kukagua ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Kishapu wasichana ambalo limetengewa kiasi cha shilingi milioni 80,
Baada ya ukaguzi mwenyekiti na wajumbe hawajaridhishwa na kasi ya mkandalasi katika ujenzi wa bweni hilo, hivyo wamemtaka mkandalasi kuongeza kasi ya ujenzi ili bweni hilo likamilike haraka ili watoto waweze kuhamia kwenye bweni hilo,
Aidha mwenyekiti amesema baada ya kikao cha tathimini kufanyika kama kudagundulika kuna makosa ya makusudi au uzembe kwa watendaji ya kukwamisha miradi ya maendeleo atachukua hatua kali kwao,
Katiaka ziara ya kamati ya Utawala, Fedha na mipango, kamati iliambatana na wataalamu wa idara tofauti tofauti.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa