Mwezeshaji kutoka kampuni ya Affluence Training Bw. Stafford Kwanama akizungumza kwenye mafunzo ya watumishi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, leo Novemba 20,2025.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wamepewa mafunzo ya elimu ya fedha na jinsi ya kukabiliana na changamoto za afya ya akili kutoka kwa waratibu wa elimu ya uwekezaji, mafunzo ya kitaalamu, na elimu sekta ya afya ya akili.

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye mafunzo ya elimu ya fedha na kukabiliana na changamoto ya afya ya akili,kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, leo Novemba 20,2025
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo leo Novemba 20,2025 yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo, Mwezeshaji wa mafunzo ya kitaalamu kutoka kampuni ya Affluence Training Bw. Stafford Kwanama, amesema watumishi wanatakiwa kuwa na maandalizi thabiti ya kustaafu wakiwa bado kazini ikiwa ni pamoja na kupanga malengo na mpango mkakati wa kujiwekea akiba binafsi ya fedha na kuiwekeza kwenye masoko ya hisa na mitaji, hati fungani za serikali na benki kuu au biashara tofauti.
“Ni jukumu la kila mmoja wetu sasa kuanza kujipanga vizuri ka kujiwekea mpango makakati wake kabla ya kustaafu ili kuwa na nidhamu ya fedha” Amesema

Mwezeshaji Bw. Kwanama akiendelea na mafunzo ya watumishi kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, leo Novemba 20,2025
Aidha, Bw. Kwanama ameeleza faida za kujiandaa kustaafu ukiwa na mapango mkakati kuwa ni kujijengea uwezo wa kujitegemea, kuimarisha afya ya mwili, akili na saikolojia, sambamba na uwekezaji wa mafao ya kustaafu kusaidia pia kizazi chake cha urithi kwa mstaafu.

Mwezeshaji kutoka Taasisi ya Serikali ya Uwekezaji ya U.T.T Bi. Magreth Tesha, akizungumza kwenye mafunzo ya watumishi uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Novemba 20,2025
Kwa upande wake, Mwezeshaji kutoka taasisi ya serikali ya uwekezaji ya U.T.T AMIS Bi. Magreth Tesha ameeleza umuhimu wa watumishi kuwekeza fedha zao kwenye mifuko mbalimbali inayoendeshwa na taasisi hiyo ili kupata faida, huku akibainisha mfuko wa hati fungani (Bond Fund) kuwa mfuko mahsusi kwa wastaafu ukiwa na gawio la kila mwezi.

Mwezeshaji Bw. Pascal Kang’iria akizungumza na watumishi kwenye mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Novemba 20,2025
Naye, Mwezeshaji mratibu wa afya ya akili kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Bw. Pascal Kang’iria amewaelimisha watumishi hao juu ya uelewa wa afya ya akili na jinsi ya kukabiliana na changamoto zake pindi zinapojitokeza.
“Mtu mmoja kati ya watu wanne wanakabiliwa na changamoto ya akili na msongo wa Mawazo”. Amesema.
Aidha Bw. Kang’iria ameeleza namna ya kukabiliana na mazingira mapya ili kuimarisha afya ya akili, sambamba na kuweza kumudu hisia bianfsi.


Watumishi wakiendelea kusikiliza mafunzo hayo ya elimu ya fedha na kukabiliana na changamoto ya afya ya akili, kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Novemba 20,2025
Elimu ya fedha na uelewa wa afya ya akili ni nguzo muhimu kwa ustawi wa watumishi wa umma na sekta binafsi. Kupitia mafunzo haya, watumishi wanaweza kuepuka madeni yasiyo ya lazima na kujenga msingi imara wa maisha ya baadaye.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa