TAARIFA YA MIRADI YA MAENDELEO INAYOENDELEA KWA ROBO YA KWANZA KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026.
1. JINA LA MRADI; Ujenzi wa shule mpya ya Awali na Msingi katika eneo la shule ya Sekondari Isoso.
Mradi huu unatekelezwa kwa kiasi cha Tsh.342,900,000/=( Milioni mia tatu arobaini na mbili na laki tisa) kutoka BOOST. Mradi huo ikiwa ni ujenzi wa shule ya awali na msingi kwa maana ya vyumba viwili (2) vya madarasa ya awali na matundu sita(6) ya vyoo, vyumba sita (6) vya madarasa ya msingi na matundu kumi(10) ya vyoo pamoja na jengo moja (1) la utawala na matundu mawili (2) ya vyoo.

Kiambatanisho Na.1: Ujenzi wa vyumba sita(6) vya madarasa ya shule ya msingi.

Kiambatanisho Na.2: Ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa ya awali na vyoo matundu sita(6).
Kiambatanisho Na. 3: Ujenzi wa jengo moja (1) la utawala na matundu mawili(2) ya vyoo.


Kiambatanisho Na.4: Ujenzi wa matundu kumi(10) ya vyoo.
2. JINA LAMRADI; Ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa na matundu sita(6) ya vyoo, katika shule ya msingi Nhobola. Mradi huu unatekelezwa kutokana na fedha za BOOST kiasi cha Tsh. 66,200,000.00 (milioni sitini na sita na laki mbili).

Kiambatanisho Na 1: Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa