• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utawala
      • Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya jamii
      • Afya
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • HUDUMA ZA SHERIA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • TEHAMA
      • Utamaduni, Sanaa na Michezo
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Usafi wa Mazingira na Udhibiti Taka
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Kilimo na Mifugo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa Halmashauri
    • Ratiba za vikao vya kisheria vya MSM
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya picha na video za shughuli za maendeleo

DC KISHAPU AWASILISHA TAARIFA YA WILAYA YA UTEKELEZAJI WA ILANI, HALMASHAURI KUU YAIBARIKI

Posted on: January 21st, 2026

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi akiwasilisha taarifa ya Wilaya ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020–2025 kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chama hicho Januari,21,2026


Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imeendelea kuonesha mafanikio makubwa katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020–2025, baada ya kufikia asilimia 48.9 ya utekelezaji katika kipindi cha Julai hadi Disemba 2025.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Shija Ntelezu akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya kishapu cha kupokea taarifa ya Wilaya ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020–2025 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chama hicho Wilaya ya Kishapu Januari,21,2026


Taarifa hiyo imewasilishwa Januari 21, 2026 na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chama hicho Wilaya ya Kishapu.


Akitoa taarifa hiyo, Mhe. Masindi amesema kuwa utekelezaji huo umetokana na ushirikiano mzuri kati ya Serikali, Chama Cha Mapinduzi pamoja na wananchi, hali iliyopelekea kukusanywa na kutekelezwa jumla ya shilingi bilioni 5.13, sawa na asilimia 48.9 ya makisio ya shilingi bilioni 10.50 yaliyopangwa kwa kipindi husika.

UTEKELEZAJI KWA SEKTA MUHIMU ZA MAENDELEO

Katika Sekta ya Afya, Wilaya ilipokea shilingi 575,000,000, ambapo hadi Disemba 2025 kiasi cha shilingi 296,984,829.84 kilikuwa kimepokelewa na kutekelezwa, fedha zilizolenga kuboresha huduma za afya na miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za tiba.

Kwa upande wa Sekta ya Elimu, jumla ya shilingi 3,978,709,752.60 zilipokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu, ambapo hadi Disemba kiasi cha shilingi 1,697,654,000 kilikuwa kimepokelewa na kutumika katika ujenzi wa madarasa, vyoo, nyumba za walimu pamoja na ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia.

Sekta ya Kilimo,
Wilaya ilipokea shilingi 72,827,836.30, fedha zilizotumika kuimarisha huduma za ugani, kuongeza uzalishaji na kuwajengea uwezo wakulima ili kuongeza tija na kipato chao.

Sekta ya Biashara na Uwekezaji, 
Wilaya ilifanikiwa kukusanya shilingi 310,694,325.00, fedha zilizotumika kuboresha mazingira ya biashara, kuongeza ajira na kukuza uchumi wa wananchi.

Aidha, kupitia Sekta ya Maendeleo ya Jamii, jumla ya shilingi 304,000,000 zilitolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mikopo ya asilimia 10, hatua iliyochangia kuinua uchumi wa kaya na makundi maalum.

Kwa upande wa Sekta ya Umeme, kiasi cha shilingi 289,193,967.36 kilitumika kupeleka na kuboresha huduma ya umeme katika maeneo ya vijijini na mijini, jambo lililorahisisha shughuli za uzalishaji na huduma za kijamii.

Sekta ya Barabara, 
Wilaya ilipokea shilingi 1,908,563,308.00, fedha zilizotumika katika ujenzi na matengenezo ya barabara ili kuboresha miundombinu ya usafiri na kurahisisha shughuli za kiuchumi ndani ya wilaya.

Pia Sekta ya Maji,Wilaya ilipokea kiasi cha shilingi 387,391,711.98 kwa ajili ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maji ndani ya Wilaya na Kata

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya Mhe. Josephati Limbe Emmanuel akifuatilia kikao hicho

Hata hivyo, Mhe. Masindi amewahimiza viongozi wa CCM na watendaji wa Serikali kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi kwa uadilifu na uwajibikaji, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano na wananchi ili kuhakikisha malengo ya Ilani ya CCM yanafikiwa kikamilifu.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu, Shija Ntelezu, amesema Chama kimeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2025.

"Taarifa hii inaonesha wazi kazi kubwa inayofanywa na Serikali chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na watendaji na wananchi. Tunawapongeza viongozi na watendaji wote kwa kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hususan katika sekta za elimu, afya, barabara na kilimo. Ni wajibu wetu kama Chama kuendelea kusimamia, kuhimiza uwajibikaji na kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa viwango vinavyokubalika.”ameongeza Ntelezu

Aidha, amewahimiza wajumbe wa CCM kuendelea kuwa mabalozi wa utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa wananchi, kwa kusikiliza kero, kutoa elimu na kuimarisha mshikamano kuelekea kukamilika kwa kipindi cha utekelezaji wa Ilani ya CCM.


Matangazo

  • TANGAZO LA MWALIKO WA MKUTANO January 20, 2026
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI December 22, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 21, 2025
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • DC KISHAPU AWASILISHA TAARIFA YA WILAYA YA UTEKELEZAJI WA ILANI, HALMASHAURI KUU YAIBARIKI

    January 21, 2026
  • SHINYANGA YAJIPIMA UTEKELEZAJI MKATABA WA LISHE NA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    January 16, 2026
  • KAMATI YA FUM KISHAPU YAKAGUA MIRADI YA ZAIDI YA TSH. B. 1.2

    January 15, 2026
  • RC MHITA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI NA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KISHAPU.

    January 10, 2026
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa