• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Nyaraka
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • Matangazo
    • Sheria ndogo ya ushuru wa huduma
    • Mifumo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
      • Uvuvi wa Samaki katika Bwawa la Songwa, Bwawa mhumbu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Mhe. William Luhende Jijimya - Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Francis Manyanda - Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Joel Ndettoson - Diwani kata ya Kishapu
      • Mhe. Mohamed Aman - Diwani kata ya Ndoleleji
      • Mhe. Lucas Nkende - Diwani kata ya Mwamashele
      • Mhe. Pontias Daud - Diwani kata ya Mwataga
      • Mhe. James Kasomi - Diwani kata ya Bubiki
      • Mhe. Bushi Mpina - Diwani kata ya Mwamalasa
      • Mhe. Nyama Kisinza - Diwani kata ya Somagedi
      • Mhe. Mashini W. Washima - Diwani kata ya Uchunga
      • Mhe. Anderson Mandia - Diwani kata ya Ukenyenge
      • Mhe. Edward Manyama - Diwani kata ya Kiloleli
      • Mhe. Reuben Siyabo - Diwani kata ya Bupigi
      • Mhe. Bujiku Nyanda - Diwani kata ya Mwaweja
      • Mhe. Michael Paul - Diwani kata ya Shagihilu
      • Mhe. Luhende S. Luhende - Diwani kata ya Lagana
      • Mhe. Richard Dominico - Diwani kata ya Talaga
      • Mhe. James Kamuga - Diwani kata ya Igaga
      • Mhe. Lameck Nsubata - Diwani kata ya Itilima
      • Mhe. Mpemba Malangahe - Diwani kata ya Bunambiyu
      • Mhe. Makenzi Charles - Diwani kata ya Busangwa
      • Mhe. Nestory Kalugula - Diwani kata ya Ngofila
      • Mhe. Lwinzi Kidiga - Diwani kata ya Maganzo
      • Mhe. Samson Gelewa - Diwani kata ya Mwasubi
      • Mhe. Sarah Marco - Diwani kata ya Idukilo
      • Mhe. Enock Bundala - Diwani kata ya Masanga
      • Mhe. Thabidha Mmbando - Diwani kata ya Mwakipoya
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri
  • miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Kituo Cha Habari
    • maktaba ya picha
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa za Vyombo vya Habari
  • Maeneo
    • Kata
      • Orodha ya Kata
    • Tarafa
      • Orodha ya Tarafa
    • Vijiji
      • Orodha ya Vijiji

DC MASINDI AHAMASISHA MAENDELEO NA UWAJIBIKAJI

Posted on: August 6th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Peter Masindi akizungumza na wananchi wa Mhunze Wilayani humo kwenye mkutano wake wa hadhara wa kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali walizonazo Agosti 6,2025 Mkutano uliofanyika Kitongoji cha Mwasele "b"

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi ameendelea kuwa faraja kwa wananchi wa Wilaya hiyo baada ya kumtua kilio mzee aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tezi dume na uvimbe kwa zaidi ya miaka miwili na kushindwa kumudu gharama za matibabu hivyo ataanza kupata huduma ya matibabu Agosti 7 mwaka huu katika Hospitali ya Dr.Jakaya Kikwete Kishapu .

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi wa Mhunze uliofanyika Kitongoji cha Mwasele "b" Mhunze, ambapo wananchi wamepata elimu juu ya fursa za mikopo ya Halmashauri, biashara, utaratibu wa kupata vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na huduma za benki, Mhe. Masindi ametumia fursa hiyo kuhimiza wananchi kutambua thamani ya muda na kujikita katika shughuli zenye tija.

“Vipo vitu vitatu ambavyo ni mhimili mkubwa kwa mwanadamu kwanza ni kujali muda, kumpenda Mungu, na pia kujali watu. Mbali na hayo, hakuna maendeleo yatakayompata mtu asiyezingatia hayo,” amesema Mhe. Masindi huku akipongeza jitihada za baadhi ya wananchi walioanza kujishughulisha na shughuli za kiuchumi.

Aidha, DC Masindi amewataka wananchi wa Kishapu kuacha kupoteza muda kwa mambo yasiyo na faida na badala yake wafanye kazi kwa bidii na kuweka akiba ili kujikwamua kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Afisa Biashara wa Wilaya ya Kishapu, Ezekiel Alphonce, ameeleza kuwa Halmashauri imetenga jumla ya shilingi milioni 100 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya kuboresha vibanda vya mnada wa Mhunze huku maboresho hayo yakijumuisha ujenzi wa vibanda vya kisasa vya biashara pamoja na vyoo vya matundu matatu katika eneo la maegesho ya magari.

Mzee Lameck Kiyaga, amempongeza Mkuu huyo kwa kutenga muda wake kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ameongeza kwa kuombauboreshaji wa vibanda vya kisasa kwenye Mnada wa Mhunze yaambatane na uwepo wa huduma ya  miundombinu ya maji, umeme na mazingira bora kwa wafanyabiashara.

Kwa upande mwingine, Mhe. Masindi amevitaka vikundi vyote vinavyodaiwa fedha na Halmashauri kuhakikisha kuwa vinamaliza madeni yao ifikapo Novemba 6, 2025 akisema kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa vikundi vitakavyokaidi agizo hilo.

Amehitimisha kwa kutoa wito kwa wananchi kuwa na uthubutu wa kuanzisha biashara na kutumia fursa zilizopo katika mnada wa Mhunze kwa maendeleo yao binafsi na ya jamii kwa ujumla.

Katika Mkutano huo Mhe Masindi amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Kishapu kujitokeza kwa wingi  kuupokea mwenge wa uhuru utakaoingia Agosti 8,2025 ukitokea Manispaa ya Shinyanga kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita huku mwenge  huo wa uhuru ukikagua,kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali Wilayani humo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bi.Fatma Mohamed akizungumza wakati akimkaribisha Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi kwenye mkutano wake wa hadhara wa kusikiliza na kutatua changamoto walizonazo wananchi wa Mhunze Mkutano uliofanyika Kitongoji cha Mwasele "b" Agosti 6,2025

Matangazo

  • TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA KWA KIPINDI KILICHOISHIA TAREHE 30 JUNE. 2022 August 14, 2023
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI November 03, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili September 20, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • JOHNSON AHAMASISHA MAPINDUZI KUWALINDA WANAWAKE NA WATOTO KISHAPU

    August 15, 2025
  • MGOMBEA UBUNGE CHAMA CHA MAKINI JIMBO LA KISHAPU ACHUKUA FOMU

    August 14, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WALIDHISHWA NA MIRADI YOTE KISHAPU

    August 08, 2025
  • KILELE CHA MAADHIMISHO WIKI YA UNYONYESHAJI KISHAPU YAFANYIKA SHAGIHILU

    August 07, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa