• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Nyaraka
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • Matangazo
    • Sheria ndogo ya ushuru wa huduma
    • Mifumo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
      • Uvuvi wa Samaki katika Bwawa la Songwa, Bwawa mhumbu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Mhe. William Luhende Jijimya - Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Francis Manyanda - Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Joel Ndettoson - Diwani kata ya Kishapu
      • Mhe. Mohamed Aman - Diwani kata ya Ndoleleji
      • Mhe. Lucas Nkende - Diwani kata ya Mwamashele
      • Mhe. Pontias Daud - Diwani kata ya Mwataga
      • Mhe. James Kasomi - Diwani kata ya Bubiki
      • Mhe. Bushi Mpina - Diwani kata ya Mwamalasa
      • Mhe. Nyama Kisinza - Diwani kata ya Somagedi
      • Mhe. Mashini W. Washima - Diwani kata ya Uchunga
      • Mhe. Anderson Mandia - Diwani kata ya Ukenyenge
      • Mhe. Edward Manyama - Diwani kata ya Kiloleli
      • Mhe. Reuben Siyabo - Diwani kata ya Bupigi
      • Mhe. Bujiku Nyanda - Diwani kata ya Mwaweja
      • Mhe. Michael Paul - Diwani kata ya Shagihilu
      • Mhe. Luhende S. Luhende - Diwani kata ya Lagana
      • Mhe. Richard Dominico - Diwani kata ya Talaga
      • Mhe. James Kamuga - Diwani kata ya Igaga
      • Mhe. Lameck Nsubata - Diwani kata ya Itilima
      • Mhe. Mpemba Malangahe - Diwani kata ya Bunambiyu
      • Mhe. Makenzi Charles - Diwani kata ya Busangwa
      • Mhe. Nestory Kalugula - Diwani kata ya Ngofila
      • Mhe. Lwinzi Kidiga - Diwani kata ya Maganzo
      • Mhe. Samson Gelewa - Diwani kata ya Mwasubi
      • Mhe. Sarah Marco - Diwani kata ya Idukilo
      • Mhe. Enock Bundala - Diwani kata ya Masanga
      • Mhe. Thabidha Mmbando - Diwani kata ya Mwakipoya
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri
  • miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Kituo Cha Habari
    • maktaba ya picha
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa za Vyombo vya Habari
  • Maeneo
    • Kata
      • Orodha ya Kata
    • Tarafa
      • Orodha ya Tarafa
    • Vijiji
      • Orodha ya Vijiji

KAMATI YA SIASA YARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MIRADI KISHAPU YAHIMIZA KASI YA UTEKELEZAJI

Posted on: June 7th, 2025

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Peter Mashenji(kushoto) na Mku wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi (kulia) wakiendelea na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo yenye lengo la kuona utekelezaji wa ilani ya CCM. 

Kamati ya siasa ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo kwa lengo la kuona utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza katika ukaguzi wa miradi hiyo Kaimu mwenyekiti wa CCM Wilaya Mhe.Peter Francis Mashenji amesema miradi yote inaridhisha katika mwenendo wa utekelezaji wake na kuongeza kuwa uko wajibu wa kuongeza kasi ili ikamilike kwa haraka huku wakizingatia ubora wa ujenzi.

Miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA

1.mradi wa maji ya Ziwa Victoria Kijiji cha Mwabusiga Kata ya Kishapu unaotekelezwa na Mkandarasi MIWI Constraction Co.Ltd ulioanza Januari 2025 na unatatajiwa kukamlika Septemba 2025 wenye tuamani ya Tsh.Milion 281,658,305 kutoka mfuko wa maji wa taifa(NWF) utakao wanufaisha Wananchi wapatao 2,415.

2.Mradi wa maji ya Ziwa Victoria Kijiji cha Ipeja Kata ya Itilima Mkandarasi wa mradi huo ni Corsyne Consult Limited muda wa mradi ni miezi 6 na utekelezaji wake unatarajia kukamilika Juni 30,2025  mpaka sasa una 98%na wananchi wameanza kupata huduma ya maji safi kupitia mradi huo.

  Gharama za mradi ni Tsh. Milion 381,742,714.50  wanufaika wa mradi huo ni wananchi wa Kijiji wapatao 1,200.

3.Mradi wa Maji ya Bomba Masanga-Ndoleleji lenye urefu wa Km 33.3 unaotekelezwa na mkandarasi Mponela Construction and Company Limited muda wa utekelezaji  mradi ni Mwaka mmoja na unatarajia kukamilika Octoba 30,2025 na sasa umefikia 75%.

  Mradi unagharama ya Tsh.Bilion 2,357,568,787 fedha kutoka serikali kuu kupitia Program ya Malipo kwa Matokea (PforR) wanufaika wa Mradi huo ni Wananchi wa Vijiji vya Ndoleleji,Masanga,Mwampalo na Ng'wang'halanga wapatao 12,768

    AFYA

1.Zahanati ya Wela ilipokea kiasi cha Tsh.Milioni 50,000,000 kutoka serikali kuu kw ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba vya Zahanati mwa mwaka 2024/2025

2.Ujenzi wa Wodi maalumu (VIP) Hospitali ya Dr.Jakaya Kikwete Halmashauri ilipokea kiasi cha Tsh. Milioni 200,000,000 kutoka serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa wodi hiyo ulioanza Disemba 1,2024 unatarajia kukamilika Juni 31,2025.

  Mradi upo hatua za ukamilishaji(Kufunga milango,kufunga mfumo wa maji safi na maji taka  pamoja na kupaka rangi mkono wa mwisho)

3.Ujenzi wa matundu 5 ya vyoo Zahanati ya Wela,Halmashauri ilipokea kiasi cha Tsh.milion 25,000,000 fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa matundu 5 ya vyoo,Placenta pit na kichomea taka.

    Mradi ulianza Machi 10,2025 na unatarajia kukamilika Julai 10,2025 ambapo hadi sasa mradi uko kwenye hatua ya lipu kwa jengo na hatua za mwisho za utendaji shimo la choo.

Miradi inayotekelezwa na TARURA

 1.ujenzi wa daraja barabara ya Igaga-Dugushilu(Tsh.Milioni 128,500,000) unatarajiwa kukamilika Julai 25,2025 Mkandalasi ni Gladiators Investment Limited

2.Dugushilu-Uchunga ujenzi wa barabara na makalavati wenye jumla ya Tsh.Milioni 154 unaotarajia kukamilika ifikapo Julai 25,2025 wenye Km 5.6.

3.Maganzo-Shinyanga Dc fedha kutoka Benki ya dunia kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Muhumbu katika Kijiji cha Ikonongo Mkandalasi akiwa ni Kihamba Constraction Company Limited.

ELIMU

Ujenzi wa Karakana Shule ya Msingi Kanawa mwaka wa fedha 2024/2025 shule ilipokea Tsh.Milioni 54,000,000 ambapo Milion 50 zitatumika kujenga karakana ya elimu ya watu wazima na milion 4 ujenzi wa matundu 2 vya choo.

Karakana hiyo imefadhiriwa na kujangwa na  Taasisis ya elimu ya watu wazima chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia kwa ufadhiri  wa watu wa Korea (KOICA)

Aidha Mashinji amesema malengo ya  miradi hiyo ni kuwasogezea huduma wananchi ili waepukane na adha mbalimbali ikiwemo wananchi kupata maji safi,salam na yenye kuwatosheleza wananchi,kupunguza na kuondoa magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo safi na salama,kutembea umbali mrefu kutafuta maji,kupata huduma za afya kwa baraka na wepesi, Uraisi wa usafiri wa kwenda kupata huduma za kijamii na kusafirisha mazao kw urahisi kwenda kwenye masoko na minada na kuwapa Vijana wa Kiume na Kike  wenye umri wa miaka 14-19  waliokatisha masomo yao katika mfumo rasmi wa elimu ya Msingi na Sekondari kwa sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa,utoro,umasikini,kufukuzwa na mimba.

"Ni kweli tumepitia miradi yote nishauri tu kasi ya utekelezwaji wake uongezeka huku  muda wa ukamilishaji miradi uzingatiwe ili wananchi wetu wapate huduma haraka iwezekanavyo hatutaki kusikia muda wa kukamilisha mradi umefika na haujakamilika mtakwamisha shughuli za maendeleo kwa wananchi wetu wa Kishapu" ameongeza Mashenji

Matangazo

  • TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA KWA KIPINDI KILICHOISHIA TAREHE 30 JUNE. 2022 August 14, 2023
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI November 03, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili September 20, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • VIJIJI 16 VINAVYOZUNGUKA MIGODI KISHAPU MIGOGORO YA ARDHI KUKOMESHWA

    June 27, 2025
  • TAKUKURU YAZINDUA JENGO JIPYA KISHAPU, LAWAPA WANANCHI IMANI NA UJASIRI KUPINGA RUSHWA

    June 26, 2025
  • DED KISHAPU AHIMIZA USHIRIKIANO KATI YA NGO's NA SERIKALI

    June 23, 2025
  • TIP YAENDESHA MAFUNZO YA KUPINGA UKATILI KISHAPU

    June 17, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa