Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi (kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Bw.Emmanuel Johnson(kushoto) katika kikao cha kuvunja kamati ya Mwenge wa Uhuru uliopita Wilayani humo mnamo Agosti 8,2025 walipokuwa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri Septemba 25,2025
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mwenge wa Uhuru Wilayani humo ametoa wito kwa Watuishi na wananchi kuhakikisha miradi yote iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru inalindwa na kuendelezwa kwa manufaa ya jamii.
Akizungumza wakati akivunja Kamati ya Mwenge Septemba 25,2025 Katika ukumbi wa Halmashauri Mhe. Masindi amesema Mwenge umekuwa chachu ya mshikamano na maendeleo, huku pia ukihimiza Watanzania kushiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025.

“Uwezo wa kujenga Taifa lenye maendeleo na mabadiliko upo mikononi mwa wananchi kupitia kuchagua viongozi bora. Ni muhimu kuendelea kuishi kwa upendo, mshikamano na kukubali matokeo ya uchaguzi kwa utulivu na amani,” amesema Mhe. Masindi.

Aidha, amesisitiza kuwa wananchi hawapaswi kushirikiana na watu wanaolenga kuleta mafarakano, bali waendelee kushirikiana kwa mshikamano na umoja ili kulinda amani ya Taifa kipindi cha uChaguzi na baada ya Uchaguzi.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi katika mapokezi na mkesha wa Mwenge wa Uhuru mwaka ujao wa 2026, huku akiwasihi watumishi washirikiane kwa upendo na mshikamano ili kuhakikisha maandalizi yanakuwa bora zaidi.

Akihitimisha hotuba yake, Mhe. Masindi amekabidhi vyeti vya pongezi kwa Kamati zote zilizoshiriki maandalizi ya Mwenge wa Uhuru pamoja na watu maalum waliotoa mchango mkubwa kufanikisha zoezi hilo.

Ikumbukwe kuwa Mwenge wa Uhuru ulipitia Jumla ya miradi saba(7) Wilayani humo ikiwemo Mwenge wa uhuru ulikagua Kikundi cha Vijana Wachapakazi kilichopo Kata ya Songwa kinatekeleza mradi wa kilimo cha nyanya kwenye ekari tano kwa mkopo wa Shilingi 20,752,209/= kutoka asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri,Mwenge huo pia umezindua na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa vyumba saba vya madarasa na matundu nane ya vyoo katika shule mpya ya sekondari ya Masagala kwa gharama ya Shilingi 196,400,000.
Mwenge huo ulizindua na kuweka jiwe la msingi mradi wa Maji uliotekelezwa na Serikali kupitia Mradi huo umehusisha ujenzi wa tenki la maji la lita 100,000, vituo vitatu vya kuchotea maji, mtandao wa bomba wa mita 2,670, uzio na alama za bomba, kwa gharama ya Shilingi milioni 445.05 kupitia Programu ya Malipo kwa Matokeo (P for R).Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imekamilisha ujenzi wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria kutoka Nyenze hadi Ng’wangh’olo Wilayani Kishapu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani.

Pia Mwenge wa Uhuru ulitembelea na kuweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Wela iliyopo Kata ya Bupigi ikiwa ni zao la jitihada za wananchi waliokuwa wakitembea zaidi ya kilomita 15 kufuata huduma za afya, ambapo mwaka 2011 walichangisha Shilingi 10,500,000/= kuanzisha ujenzi huo.Serikali kupitia Serikali Kuu na mapato ya ndani ya Halmashauri imechangia Shilingi 75,000,000/= kukamilisha ujenzi huo unaojumuisha jengo la zahanati, vyoo matundu matano, kichomea taka na Placenta Pit.Mradi huu wenye thamani ya Shilingi 85,500,000/= unatarajiwa kuhudumia wananchi zaidi ya 7,600 wa Kata ya Bupigi na Vijiji jirani.
Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 ulikagua na kuweweka jiwe la msingi katika bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Mwamashele mradi ulianzishwa na wananchi mwaka 2019 kwa lengo la kuwalinda watoto wa kike dhidi ya changamoto za umbali mrefu, mimba za utotoni, unyanyasaji na utoro.Mradi huo unathamani ya Shilingi 88,105,200/=
Mwenge wa Uhuru uliweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya DED - DC yenye urefu wa kilomita 1 kwa kiwango cha lami nyepesi (DSD), mradi unaogharimu zaidi ya shilingi milioni 688. Mradi huo unatekelezwa na TARURA pamoja na Mradi wa mwekezaji Mzawa Wilayani humo Mradi wa Kituo cha mafuta cha Bin Salum.







Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa