Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi Tarafa ya Mondo Agosti 27,2025
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi amewataka wagombea wote wa Jimbo la Kishapu wanaoelekea kuanza kampeni za uchaguzi kutumia lugha ya heshima na sera zenye kujenga badala ya matusi au kejeli wanapokuwa jukwaani.
Akizungumza Agosti 27, 2025 katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Tarafa ya Mondo,Masindi amesema siasa za matusi hazina tija, na kuwakumbusha wagombea kwamba kuna maisha baada ya uchaguzi, hivyo hakuna sababu ya kuchochea uhasama.
“Wananchi wanataka kusikia sera zinazogusa maisha yao na namna mtakavyoboresha huduma za kijamii. Huu sio muda wa matusi wala kejeli. Tufanye siasa zenye heshima na staha,” amesema Masindi.
Aidha, amewataka wananchi kusikiliza kwa makini sera za wagombea na kufanya maamuzi sahihi ifikapo Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa msingi wa maendeleo upo mikononi mwao. Vilevile, Masindi amewahimiza wananchi kuendelea kuchangamkia fursa za kiuchumi, kufanya kazi kwa bidii, kuishi kwa nidhamu na kumtanguliza Mungu katika kila jambo.
Afisa Tarafa ya Mondo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Atka Faki akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi Agosti 27,2025
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wazazi pia kuhakikisha wanalea watoto wao kwenye maadili, nidhamu na ujasiri ili wawe nguzo ya maendeleo ya jamii.
Katika wito wake kwa jamii, amewahimiza kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo ikiwemo uanzishaji wa maboma ya madarasa, nyumba za walimu, vituo vya afya pamoja na kulinda miundombinu ya maji na umeme iliyowekwa kwa manufaa ya wananchi.
Mbali na hayo, amewahimiza watendaji wa Halmashauri na wakuu wa taasisi zingine za Umma na za fedha kuhakikisha wanafanya kazi kwa maslahi ya wananchi na kuwasogezea huduma muhimu ambazo serikali imekusudia kuwafikishia.
Aidha, wananchi wameelimishwa kuhusu huduma za mikopo zinazotolewa na Halmashauri na Taasisi ya Kifedha (CRDB), huku wakihimizwa kuchangamkia fursa hizo ili kuepuka kuingia kwenye mikopo isiyo rasmi inayochochea migogoro ya kifamilia.
Mhe.Masindi amehitimisha ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika tarafa ya Mondo Vijiji vya Nyasamba Kata ya Bubiki, Mwajiningu Kata ya Busongwa,Itongoitale Kata ya Mwasubi pamoja na Kijiji cha Idukilo Kata ya Idukilo.
Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi wa kusikiliza na kutatua kero kwa wananchi katika Kijiji cha Nyasamba kilichoko Kata ya Bubiki Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Agosti 27,2025
Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi wa kusikiliza na kutatua kero kwa wananchi katika Kijiji cha Mwajiningu Kata ya Busongwa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Agosti 27,2025
Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi wa kusikiliza na kutatua kero kwa wananchi katika Kijiji cha Itongoitale Kata ya Mwasubi Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Agosti 27,2025
Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi wa kusikiliza na kutatua kero kwa wananchi katika Kijiji cha Idukilo Kata ya Idukilo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Agosti 27,2025
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa