Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw.Emmanuel Johnson akizungumza na watumishi wa makao makuu wa Halmashauri hiyo kwenye kikao Cha kawaida Oktoba 24,2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu,Mkoani Shinyanga Bw Emmanuel Johnson ametoa wito kwa watumishi wote wa Halmashauri hiyo kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza Oktoba 24 2025,katika kikao cha kawaida kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo,Johnson amewahimiza watumishi kutumia haki yao ya kikatiba kwani Uchaguzi ni ishara ya wananchi kujitambua na kuwa huru.

Aidha amewasihi watumishi wote kuendelea kuhimiza amani na utulivu katika jamii, akiwataka kuepuka makundi yenye nia ya kuvuruga amani ya nchi.

“Tuendelee kuhimiza Wananchi kulinda amani ya nchi yetu hasa kundi vijana ambao ndio wamekuwa wakiingizwa na kujiingiza kwenye uharibifu mkubwa wa kuchechea uvunjifu wa Amani na tuwahimize wanaowajibu wa kuilinda kwani amani haijaribiwi kwa kupotea,” amesisitiza.

Amewataka watumishi kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii kwa kuonesha nidhamu, uzalendo na uwajibikaji wakati wa mchakato wa uchaguzi, akihimiza kila mtumishi kushiriki kikamilifu bila kuvunja sharia wala kujiingiza kwenye makundi ya siasa.

Johnson amehitimisha kwa kuwatakia kila la heri watumishi wote katika maandalizi ya uchaguzi, akiwakumbusha kuwa baada ya zoezi la upiagji kura kisha warejee majumbani kwao na kusubiria kwa utulivu matokea kutangazwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika kote nchini Tanzania, huku viongozi wakiendelea kuhimiza ushiriki wa wananchi na kulinda amani katika kipindi chote cha uchaguzi.

Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa