• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Nyaraka
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • Matangazo
    • Sheria ndogo ya ushuru wa huduma
    • Mifumo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
      • Uvuvi wa Samaki katika Bwawa la Songwa, Bwawa mhumbu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Mhe. William Luhende Jijimya - Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Francis Manyanda - Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Joel Ndettoson - Diwani kata ya Kishapu
      • Mhe. Mohamed Aman - Diwani kata ya Ndoleleji
      • Mhe. Lucas Nkende - Diwani kata ya Mwamashele
      • Mhe. Pontias Daud - Diwani kata ya Mwataga
      • Mhe. James Kasomi - Diwani kata ya Bubiki
      • Mhe. Bushi Mpina - Diwani kata ya Mwamalasa
      • Mhe. Nyama Kisinza - Diwani kata ya Somagedi
      • Mhe. Mashini W. Washima - Diwani kata ya Uchunga
      • Mhe. Anderson Mandia - Diwani kata ya Ukenyenge
      • Mhe. Edward Manyama - Diwani kata ya Kiloleli
      • Mhe. Reuben Siyabo - Diwani kata ya Bupigi
      • Mhe. Bujiku Nyanda - Diwani kata ya Mwaweja
      • Mhe. Michael Paul - Diwani kata ya Shagihilu
      • Mhe. Luhende S. Luhende - Diwani kata ya Lagana
      • Mhe. Richard Dominico - Diwani kata ya Talaga
      • Mhe. James Kamuga - Diwani kata ya Igaga
      • Mhe. Lameck Nsubata - Diwani kata ya Itilima
      • Mhe. Mpemba Malangahe - Diwani kata ya Bunambiyu
      • Mhe. Makenzi Charles - Diwani kata ya Busangwa
      • Mhe. Nestory Kalugula - Diwani kata ya Ngofila
      • Mhe. Lwinzi Kidiga - Diwani kata ya Maganzo
      • Mhe. Samson Gelewa - Diwani kata ya Mwasubi
      • Mhe. Sarah Marco - Diwani kata ya Idukilo
      • Mhe. Enock Bundala - Diwani kata ya Masanga
      • Mhe. Thabidha Mmbando - Diwani kata ya Mwakipoya
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri
  • miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Kituo Cha Habari
    • maktaba ya picha
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa za Vyombo vya Habari
  • Maeneo
    • Kata
      • Orodha ya Kata
    • Tarafa
      • Orodha ya Tarafa
    • Vijiji
      • Orodha ya Vijiji

JAMII KISHAPU YASISITIZWA KUHIFADHI MAZINGIRA KWA VITENDO

Posted on: June 5th, 2025

Katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, jamii ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga imetakiwa kuchukua hatua za dhati katika kulinda mazingira ikiwemo kupanda miti na kufanya usafi kwenye maeneo ya makazi na huduma za kijamii.

Maadhimisho hayo yalifanyika Juni 5,2025 katika Kijiji cha Mwigumbi, Kata ya Mondo, yakiongozwa na Severini Musyangi, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wa tukio hilo.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Severini Musyangi akikabidhi cheti cha pongezi Meneja mradi wa umeme jju-Ngunga  Bw.Daniel Xu Juni 5,2025 kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira yaliyofanyika Kijiji cha Mwigumbi Kata ya Mondo ngazi ya Wilaya

Akizungumza na wananchi na wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Mwigumbi Musyangi amesisitiza kuwa kila mwananchi ana wajibu wa moja kwa moja katika kulinda mazingira, huku akipendekeza mpango wa kila mwanafunzi kupanda mti mmoja kila mwanzo wa mwaka na kuuhudumia hadi unakomaa.

“Kila mwanafunzi anapaswa kupanda mti mmoja na kuuhudumia. Vivyo hivyo, kila mwananchi ahakikishe anapanda miti katika maeneo yake ya makazi na si kusubiria serikali ama mashirika yasiyokuwa ya serikali kupanda ” amesema Musyangi .

Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Kishapu Charles Kanwakabo amesema maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika katika eneo la Mwigumbi kutokana na wingi wa watu, hali inayochochea uwezekano wa uharibifu wa mazingira ikiwa hakuna elimu na usimamizi thabiti.

“Tumechagua Mwigumbi kwa sababu kuna msongamano wa watu Tumeweza kupanda miti 300 ya matunda na ya kivuli sambamba na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya umma hivyo tunaamini kupitia ushirikiano wa jamii na maafisa wetu wa afya kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Wilaya elimu hii itasaidia kudhibiti uharibifu wa mazingira,” amesema Kanwakabo.

Maadhimisho hayo yalihusisha ushiriki wa wananchi, viongozi wa Vijiji, wanafunzi, watumishi wa Halmashauri pamoja na wadau wa mazingira, ambapo shughuli mbalimbali za kijamii kama upandaji miti na kampeni ya kupinga matumizi ya plastiki zilifanyika.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi Lidya Boniphace mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Ng’wigumbi amesema kuwa wanafundishwa masomo kuhusu mazingira shuleni ikiwa ni sehemu ya kuandaa kizazi kinachojali na kuhifadhi mazingira.

“Tumejifunza namna ya kupanda miti, nyasi na pia kuepuka matumizi ya plastiki tunajua ni jukumu letu kutunza mazingira ya sasa na ya baadaye,” amesema kwa kujiamini.

Afisa mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Charles Kanwakabo akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika Kijiji cha Mwigumbi  Kata ya Mondo juni 5,2025 kwa ngazi ya Wilaya

Kaulimbiu ya Mwaka 2025: “Rekebisha Ardhi kwa Mustakabali Endelevu” ikilenga kurejesha uoto wa asili, kuboresha matumizi ya ardhi, na kuhimiza jamii duniani kote kuchukua hatua za kuzuia mmomonyoko wa ardhi na mabadiliko ya tabianchi hivyo Wilaya ya Kishapu imedhihirisha kuwa kwa kutumia elimu na ushiriki wa wananchi, malengo haya yanaweza kufikiwa kwa vitendo.

Kishapu ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na changamoto ya ukame, mmomonyoko wa ardhi, na ukataji miti hovyo kwa matumizi ya kuni. Kwa hivyo, hatua ya kuhamasisha kila mwanafunzi kupanda mti ni ya kimkakati inalenga kujenga mazoea mapema ya kuhifadhi mazingira.

Aidha msisitizo kwenye elimu mashuleni kuhusu mazingira na kushirikisha jamii nzima ni hatua endelevu itakayosaidia kulinda vyanzo vya maji, kuimarisha hali ya hewa na kuzuia athari za mabadiliko ya tabianchi ambazo zimeanza kushuhudiwa pia katika mkoa wa Shinyanga.

Maadhimisho hayo yameambatana na Mgeni rasmi kutoa vyeti vya pongezi kwa wadau wa mazingira wakiwemo Wdl,Tcrs,Sinohydro, Daniel Xu, Nmb Kishapu pamoja na Crdb banc Maganzo.

Matangazo

  • TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA KWA KIPINDI KILICHOISHIA TAREHE 30 JUNE. 2022 August 14, 2023
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI November 03, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili September 20, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • JAMII KISHAPU YASISITIZWA KUHIFADHI MAZINGIRA KWA VITENDO

    June 05, 2025
  • SERIKALI YATOA CHANJO ZA MIFUGO KWA RUZUKU KATIKA WILAYA YA KISHAPU

    June 04, 2025
  • SERIKALI KISHAPU YAZUIA TANI 30 ZA PAMBA ZILIZOPIMWA KINYUME NA TARATIBU

    June 04, 2025
  • DC MASINDI ATAKA WAUGUZI KISHAPU WAFANYE KAZI KWA NIDHAMU NA UPENDO

    May 31, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa