Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, CP. Salum Hamduni, amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi wa umma pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali.

Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Fatma Mohamed.
Katika kikao hicho kilichofanyika Mei 7,2025 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo watumishi waliwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi kila siku pamoja na uhitaji wa mafunzo kazini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson.
Cp. Hamduni ametoa utatuzi wa baadhi ya changamoto na kuahidi kushughulikia changamoto zingine kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu, Bw. Emmanuel Johnson, amempongeza Katibu Tawala licha ya kuwa na kazi nyingi za kiutendaji na bado ametenga muda wake kuja kusikiliza changamoto za watumishi.
"Umekuwa kiongozi Bora na mfano mzuri ambao na sisi tunapaswa kujifunza, umeonesha dhamira ya dhati ya kuboresha utendaji kazi na utoaji huduma kwa wananchi,” amesema Bw. Johnson.

Ziara hiyo ni sehemu ya mikakati ya ufuatiliaji na usimamizi wa utendaji kazi wa watumishi wa umma katika Mkoa wa Shinyanga.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa