Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi akiwa ndie mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani ngazi ya Wilaya yaliyofanyika Viwanja vya Zahanati ya Shagihilu Wilayani humo Agosti 7,2025
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masindi ameongoza kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani ngazi ya Wilaya, yaliyofanyika Agosti 7, 2025 katika viwanja vya Zahanati ya Shagihilu.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mhe. Masindi ametoa wito kwa jamii kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa mama na mtoto ili kuimarisha afya kupitia unyonyeshaji wa maziwa ya mama, ambao ni muhimu kwa lishe bora na kinga ya mtoto.
Amesisitiza kuwa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo na kuendelea hadi miaka miwili ni njia bora ya kupambana na udumavu na utapiamlo kwa watoto, akibainisha kuwa Wilaya ya Kishapu imeendelea kutoa elimu ya lishe bora kupitia wataalamu wa afya.
Kwa upande wake, Afisa Lishe wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Yusuph Hamis ameeleza kuwa mtoto anatakiwa anyonyeshwe ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa, na kupewa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ili kupata kinga dhidi ya maradhi.

Afisa Lishe wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Yusuph Hamis
Wananchi wa Kijiji cha Shagihilu wamepongeza elimu waliyoipata na kuahidi kuwa mabalozi wa kuisambaza katika jamii, ili kuhakikisha watoto wanapata mwanzo bora wa maisha kupitia unyonyeshaji.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Thamini Unyonyeshaji: Weka Mazingira Wezeshi kwa Mama na Mtoto.”

Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa