Mwezeshaji kutoka Idara ya Mipango na Uratibu ambaye pia ni Afisa bajeti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga James Zacharia Zitto Septemba 26,2025 akizungumza kwenye mafunzo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri hiyo
Maafisa bajeti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wameaswa kuzingatia miongozo katika maandalizi ya mipango na bajeti ili kuhakikisha utekelezaji bora wa shughuli za maendeleo za kila siku.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Septemba 26,2025 yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri hiyo,Mwezeshaji kutoka Idara ya Mipango na Uratibu ambaye pia ni Afisa bajeti wa Halmashauri hiyo James Zacharia Zitto amesema maandalizi hayo lazima yaendane na Dira ya Taifa ya Maendeleo, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa muda wa kati pamoja na sera za kitaifa.

Zitto amesisitiza umuhimu wa kuchagua malengo yanayotekelezeka na kuonyesha uhalisia wa taasisi ilipo pamoja na mwelekeo wa maendeleo unaotarajiwa.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamehusisha Maafisa bajeti kutoka Divisheni na Vitengo vyote wa Halmashauri hiyo.




Mafunzo yakiendelea

Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa