• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utawala
      • Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya jamii
      • Afya
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Tehama
      • Utamaduni, Sanaa na Michezo
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Usafi wa Mazingira na Udhibiti Taka
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Kilimo na Mifugo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa Halmashauri
    • Ratiba ya vikao vya kisheria vya MSM
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya picha na video za shughuli za maendeleo

MITI 1,500 YAPANDWA KISHAPU KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS MHE. SAMIA ZA UTUNZAJI MAZINGIRA

Posted on: January 27th, 2026

Katibu Tawala Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya hiyo ambae alikuwa mgeni rasmi kwenye zoezi a upandaji miti 1,500 katika Shule ya Msingi Isoso, Kata ya Kishapu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Januari 27,2026


Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imepanda jumla ya miti 1,500 katika Shule ya Msingi Isoso, Kata ya Kishapu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, yenye kauli mbiu isemayo "Uzalendo ni kutunza mazingira, shiriki kupanda miti".


Akizungumza kwa niaba ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Bi. Fatma H. Mohamed, amesema upandaji wa miti ni suala la msingi katika kulinda mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuhakikisha kizazi cha sasa na kijacho kinaishi katika mazingira salama na endelevu.

Fatma amebainisha kuwa maadhimisho hayo yamebeba ujumbe mahsusi wa kuenzi maono ya Rais Samia ya kulinda mazingira na kuhimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika upandaji na utunzaji wa miti, akisisitiza kuwa kupanda mti mmoja ni kuwekeza maisha ya baadaye.

Kwa upande wake Mhifadhi  Misitu  wilayani humo, Tumaini Masatu amesema wakala huo umeendelea kuwa mstari wa mbele katika kampeni za uhifadhi wa misitu na utoaji wa elimu ya mazingira, hususa kwa wanafunzi ili kujenga kizazi chenye uelewa na uwajibikaji wa mazingira.

Masatu amefafanua kuwa miti iliyopandwa itasaidia kuboresha mazingira ya shule, kutoa kivuli, kupata matunda, kupunguza athari za ukame pamoja na kuongeza uelewa wa wanafunzi juu ya umuhimu wa rasilimali za misitu.


Naye Mkuu wa Shule ya Msingi Isoso Gilbert Mtunguja ameushukuru uongozi wa Wilaya na TFS kwa kuchagua shule hiyo kuwa sehemu ya maadhimisho, akiahidi kuwa shule itahakikisha miti yote iliyopandwa inatunzwa ipasavyo.


Maadhimisho hayo yamehitimishwa kwa zoezi la pamoja la upandaji miti likiwahusisha Wananachi,Viongozi,Wakuu wa Taasisi, Watumishi wa Halmashauri, TFS, Walimu na Wanafunzi, ikiwa ni ishara ya mshikamano na dhamira ya dhati ya kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda na kuhifadhi mazingira nchini yakiambatana na kauli mbiu isemayo "Uzalendo ni kulinda mazingira, shiriki kupanda miti".Mhifadhi  Misitu Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, Tumaini Masatu akizungumza kwenye zoezi a upandaji miti 1,500 katika Shule ya Msingi Isoso, Kata ya Kishapu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Januari 27,2026


Matangazo

  • TANGAZO LA MWALIKO WA MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI January 20, 2026
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI December 22, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 21, 2025
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • VIKUNDI 21 MAKUNDI MAALUMU VYAPATIWA MIKOPO KISHAPU

    January 29, 2026
  • BARAZA LA MADIWANI KISHAPU LAAZIMIA SOKO HURIA LA PAMBA, LATOA MSISITIZO WA LISHE NA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    January 28, 2026
  • DED KISHAPU AKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA KUWAWEZESHA WAALIMU WENYE CHANGAMOTO YA UONI

    January 28, 2026
  • BARAZA LA MADIWANI KISHAPU LAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA ZA KATA ROBO YA PILI 2025/2026

    January 27, 2026
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa