Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw.Emmanuel Johnson
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw. Emmanuel Johnson, amewatakia kila la heri Wanafunzi wa darasa la saba wanaotarajia kufanya Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi unaotarajiwa kufanyika Septemba 10–11, 2025.
Bw. Johnson amesema jumla ya Shule 125 zinashiriki mtihani huo, ambapo shule za Serikali ni 122 na binafsi 3. Watahiniwa wote ni 7,195 wakiwemo wavulana 2,930 na wasichana 4,265 huku kukiwa na jumla ya mikondo 333.
Johnson amewataka Wanafunzi kutumia maarifa na mbinu walizojifunza Darasani kwa kujiamini ili waweze kufanya vizuri katika mtihani huo na kufanikisha malengo yao ya kielimu . Vilevile, amewasihi Wazazi na Walezi kuwapa Watoto utulivu, malezi chanya na msaada wa kisaikolojia katika kipindi hiki muhimu cha mtihani.
"Ni matumaini yangu Mungu atawasimamia wote kisha mtafaulu na kuendelea na masomo ya juu zaidi"ameongeza
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa