
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson(kushoto) Akimkabidhi kanuni za kudumu za utendaji katika Baraza hilo Mtendaji wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Kishapu Godwin Everygist (kulia).
Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Kishapu limezinduliwa rasmi Mei 6, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw. Emmanuel Johnson katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na chama.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Willium Jijimya (kushoto)akimkabidhi kanuni za kudumu za utendaji Mwenyekiti wa Baraza la Mamlaka Mhe.Fabian Makongo (kulia).
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Johnson amesema Kishapu ilitangazwa kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo tangu mwaka 2004 lakini utekelezaji wake ulikwamishwa na changamoto za kiuchumi.

Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Eugine Soka.
Johnson amesema hatua ya sasa imewezekana kutokana na jitihada za pamoja za viongozi na wananchi waliokubali mageuzi muhimu, ikiwemo kupunguza idadi ya vitongoji.

"Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu inasisitiza ushirikiano,uwajibikaji na kujituma kwa maslahi ya wananchi hivyo mkafanye kazi" Ameongeza Mkurugenzi Johnson

Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Eugine Soka amewapongeza kwa hatua hiyo na kusema uzalendo wa viongozi walioteuliwa ni chachu ya kuleta mabadiliko ya haraka.

Mtendaji wa Mamlaka hiyo ya Mji Mdogo Godwin Everygist, ameeleza kuwa mpango wa awali ni kuboresha miundombinu, mazingira, na usimamizi wa ujenzi unaozingatia sheria,kanuni na taratibu ili kufikia hadhi ya kuwa Halmashauri ya Mji kamili.

Mwenyekiti wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Kishapu Mhe.Fabian Makongo(kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Dionis Makala(kushoto)
Baraza hilo lina jumla ya wajumbe 17 na linaongozwa na Mhe. Fabian Makongo (Mwenyekiti) na Mhe. Dionis Makala (Makamu Mwenyekiti).

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Shika Ntelezu akizungumza kwenye uzinduzi wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Kishapu.
Mamlaka ya Mji Mdogo Kishapu sasa inaanza safari yake rasmi huku msukumo ukiwa ni kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi kwa ukaribu na kwa kasi.


Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa