Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mohamed Mhita amefanya ziara ya kikazi Wilayani Kishapu Mkoani humo kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Peter Masindi (kulia)akimkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Mboni Mohamed Mhita kwenye ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na watumishi wa umma na wakuu wa taasisi na sekta Julai 22,2025
Katika ziara hiyo, Mhe. Mhita ametembelea miradi kadhaa inayotekelezwa kwa fedha za Serikali Kuu,wadau wa maendeleo na mapato ya ndani ikiwa ni sehemu ya tathmini ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo sambamba na kujionea namna fedha za umma zinavyotumika.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mohamed Mhita akizungumza na watumishi baadhi wa Wilaya ya Kishapu katika ziara yake ya kikazi Julai 22,2015 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Miradi aliyotembelea ni pamoja na Elimu,Afya,Maji na Barabara.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Peter Masindi
Baada ya ukaguzi miradi, Mhe. Mhita amezungumza na watumishi wa Halmashauri ya Kishapu ambapo amewataka kufanya kazi kwa bidii, weledi na kwa uadilifu mkubwaa huku akisisitiza kuwa mtumishi wa umma ni kioo cha Serikali kwa wananchi, hivyo ni wajibu wao kusikiliza na kushughulikia kero za wananchi kwa wakati badala ya kusubiri malalamiko yafike ngazi za juu.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Peter Masindi (kushoto) na Katibu Tawala Wilayani humo Bi.Fatma Mohamed(kulia)
“Hatutaki kusikia mwananchi anakaa miezi kadhaa bila kupatiwa huduma kwa sababu ya uzembe wa mtumishi kuweni wasikivu, fanyeni kazi zenu kwa moyo wa kujituma na kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni,” a mesema Mhe. Mhita.
"Nimejionea Mkuu wa Wilaya rafiki yangu Masindi na Mkurugenzi wangu Johnson hakika mnafanya kazi kubwa na hii ndio furaha ya Rais wetu Mhe.Samia Suluhu Hassan endeleeni kufanya kazi kwa ajili ya Watanzania" amesema Mhita

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga BW. Emmanuel Johnson
Ametoa maagizo kwa Halmashauri hiyo kuhakikisha inaweka mikakati thabiti ya kuongeza mapato ya ndani kwa njia rafiki na kushirikiana na wafanyabiashara na wadau wengine ili kuongeza mapato yatakayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo bila kutegemea zaidi rasilimali kutoka Serikali Kuu.

“Tunataka mabadiliko yanayoonekana Kishapu iwe mfano wa namna bora ya ukusanyaji wa mapato kwa njia rafiki na jumuishi huku mkiibua vyanzo vipya vya mapato kwani huu ni mkoa wenye fursa nyingi, tuzitumie vizuri kwa maendeleo ya watu wetu,” ameongeza.

Mhe. Mhita pia ameahidi kuwa ofisi yake itaendelea kushirikiana na Halmashaur ya Kishapu ili kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati na ile ya maendeleo inakamilika kwa wakati ili iweze kuwanufaisha wananchi wakiwa ndio walengwa.


Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa