
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Paul Chacha (Kushoto) akimkabidhi hati ya makabidhiano Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mohamed Mhita (Kulia) katika Viwanja vya Stendi ya Mabasi Kagongwa Kata ya Kagongwa Wilayani Kahama Agosti 8,2025
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mohamed Mhita, leo Agosti 3, 2025, amepokea rasmi Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paul Chacha, katika viwanja vya Stendi ya Mabasi Kagongwa, wilayani Kahama.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Peter Masindi akiwa ameshikilia mwenge wa uhuru uliipokelewa ki Mkoa Stendi ya mabasi Kagongwa Kata ya Kagongwa Wilayani Kahama Mkoani humo kutoka Mkoa wa Tabora Agosti 8,2025
Akizungumza baada ya kupokea Mwenge huo, Mhe.Mhita amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Shinyanga utakimbizwa umbali wa kilomita 819.2 katika Halmashauri sita za Mkoa huo, ambapo utapitia jumla ya miradi 44 kwa ajili ya kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi.

Katibu Tawala Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Bi.Fatma Mohamed akisalimiana na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2025 Ismail Ali Ussi katika Viwanja vya stand ya mabasi Kagongwa Kata ya Kagongwa Wilayani Kahama wakiingia Mkoani humo kutokea Mkoani Tabora Agosti 3,2025
Mhita Ameeleza kuwa thamani ya miradi hiyo ni Shilingi bilioni 17.3, ikiwa ni ishara ya juhudi za Serikali katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw.Emmanuel Johnson akisalimiana na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2025 Ismail Ali Ussi katika Viwanja vya stand ya mabasi Kagongwa Kata ya Kagongwa Wilayani Kahama wakiingia Mkoani humo kutokea Mkoani Tabora Agosti 3,2025
Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu zinakimbizwa na wakimbiza Mwenge sita wakiongozwa na kiongozi wa mbio hizo, Ismail Ali Ussi.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025 ni "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu", ikisisitiza umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu kwa njia ya amani na utulivu.
Mwenge wa Uhuru unaanza mbio zake Wilayani Kahama hii Leo na unatarajiwa kukamilisha mbio zake katika Mkoa wa Shinyanga kwa Wilaya ya Kishapu na kukabidhiwa kwa Mkoa wa Simiyu Agosti 9, 2025 katika Kijiji cha Njiapanda huku mapokezi ya Wilaya ya Kishapu yatakuwa katika uwanja wa Kijiji cha Seseko na eneo la mkesha kuwa Uwanja wa Shirecu.
Mwenge huo unatarajiwa kuhamasisha mshikamano wa kitaifa, maendeleo endelevu, na ushirikiano baina ya Serikali na wananchi katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa