• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Nyaraka
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • Matangazo
    • Sheria ndogo ya ushuru wa huduma
    • Mifumo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
      • Uvuvi wa Samaki katika Bwawa la Songwa, Bwawa mhumbu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Mhe. William Luhende Jijimya - Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Francis Manyanda - Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Joel Ndettoson - Diwani kata ya Kishapu
      • Mhe. Mohamed Aman - Diwani kata ya Ndoleleji
      • Mhe. Lucas Nkende - Diwani kata ya Mwamashele
      • Mhe. Pontias Daud - Diwani kata ya Mwataga
      • Mhe. James Kasomi - Diwani kata ya Bubiki
      • Mhe. Bushi Mpina - Diwani kata ya Mwamalasa
      • Mhe. Nyama Kisinza - Diwani kata ya Somagedi
      • Mhe. Mashini W. Washima - Diwani kata ya Uchunga
      • Mhe. Anderson Mandia - Diwani kata ya Ukenyenge
      • Mhe. Edward Manyama - Diwani kata ya Kiloleli
      • Mhe. Reuben Siyabo - Diwani kata ya Bupigi
      • Mhe. Bujiku Nyanda - Diwani kata ya Mwaweja
      • Mhe. Michael Paul - Diwani kata ya Shagihilu
      • Mhe. Luhende S. Luhende - Diwani kata ya Lagana
      • Mhe. Richard Dominico - Diwani kata ya Talaga
      • Mhe. James Kamuga - Diwani kata ya Igaga
      • Mhe. Lameck Nsubata - Diwani kata ya Itilima
      • Mhe. Mpemba Malangahe - Diwani kata ya Bunambiyu
      • Mhe. Makenzi Charles - Diwani kata ya Busangwa
      • Mhe. Nestory Kalugula - Diwani kata ya Ngofila
      • Mhe. Lwinzi Kidiga - Diwani kata ya Maganzo
      • Mhe. Samson Gelewa - Diwani kata ya Mwasubi
      • Mhe. Sarah Marco - Diwani kata ya Idukilo
      • Mhe. Enock Bundala - Diwani kata ya Masanga
      • Mhe. Thabidha Mmbando - Diwani kata ya Mwakipoya
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri
  • miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Kituo Cha Habari
    • maktaba ya picha
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa za Vyombo vya Habari
  • Maeneo
    • Kata
      • Orodha ya Kata
    • Tarafa
      • Orodha ya Tarafa
    • Vijiji
      • Orodha ya Vijiji

TAKUKURU YAZINDUA JENGO JIPYA KISHAPU, LAWAPA WANANCHI IMANI NA UJASIRI KUPINGA RUSHWA

Posted on: June 26th, 2025

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Bw.Chrispin Francis Chalamila akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la ofisi hiyo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Juni 25, 2025

Wananchi Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wamepongeza jitihada za serikali ya awamu ya sita za ujenzi miundombinu ya jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani humo.

Pongezi hizo zimetolewa Juni 26,2025  baada ya uzinduzi wa jengo lenye thamani ya Tsh.Milion 438 lilolofanywa Juni 25,2025 na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU  Bw.Crispin Francis Chalamila.

Bw.Amos Masunga mkaazi wa mtaa wa Mwasele 'B' amesema uwepo wa jengo la Taasisi hiyo usiwe sababu ya utoaji elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya upingaji rushwa na mahali wanapopaswa kupeleka malalamiko yao pindi wanapokosa huduma zilizo haki zao kisheria wakihitajika kutoa Rushwa.

"Jengo hili linafaida zaidi kwetu wananchi endapo TAKUKURU watafanya kazi zao kwa mwongozo waliowekewa hivyo watoke ofsini na kuwandea  wananchi ili kuwaelimisha kuhusu maana ya Rushwa na viashiria vya rushwa hasa kundi la wanawake na wasichana wanaokutana na changamoto zaidi ya kuombwa rushwa ya ngono ili wapate kazi na wengine kupandishwa cheo"ameongeza Masunga.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Chrispin Francis Chalamila amesema uwepo wa jengo hilo ni hatua kubwa ya kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa ngazi ya jamii.

“Serikali ya Awamu ya Sita imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za TAKUKURU kote nchini hivyo tunatambua umuhimu wa taasisi hii, na ni jukumu la kila mwananchi kulitumika jengo hili kwa kutoa taarifa kuhusu viashiria au vitendo vya rushwa iliyo adui mkubwa wa maendeleo ya taifa letu,” amesema Chalamila.

Amesisitiza umuhimu wa kuchagua wagombea waadilifu kwa kuwa hao ndio watakaoshirikiana na wananchi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo katika kuleta maendeleo ikiwa kura ni tiketi ya maendeleo na uwajibikaji.

“Tukikubali kupokea rushwa kutoka kwa wagombea, ni sawa na kukataa maendeleo yetu wenyewe. Mara nyingi waliotoa rushwa hushindwa kuwajibika ipasavyo na badala yake hutanguliza maslahi yao binafsi,” ameongeza.

Amehimiza maafisa wa TAKUKURU kuongeza mbinu za ushirikishaji jamii kwa njia ya elimu, vikundi vya sanaa, na klabu mashuleni ili kuongeza uelewa kuhusu madhara ya rushwa.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo, ameipongeza serikali kwa mpango wake wa dhati wa kuimarisha taasisi hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.

“TAKUKURU ni chombo cha haki kwa wananchi. Tunaposhuhudia nidhamu ikirejeshwa miongoni mwa watumishi na wafanyabiashara, tunapata matumaini ya taifa lenye uwajibikaji na maendeleo na hii itaongeza ufanisiwa utendaji kazi kwa watumishi wa Taasisi hii kwa kuboreshewa mazingira ya kazi zao,” amesema Butondo.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, amesema jengo hilo ni kichocheo cha haki na uwazi katika jamii, huku akiwataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kupinga rushwa kwa kutoa taarifa kwa wakati.

“Tunawashukuru sana TAKUKURU kutuheshimisha kwa kutujengea jengo hili hapa Kishapu ni hatua ya kupongezwa hivyo Wananchi mnapaswa kutumia fursa hii kwa kutoa taarifa na sasa tumeboreshewa usiri tofauti na hapo awali kutokana na mazingira ya ofisi ombi langu muendelee kuelimishwa kuhusu rushwa hasa tunapoelekea uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani,” amesema Masindi.

Mkurugenzi wa Hati Milki wa TAKUKURU, Eng. Dkt. Emmanuel Kiyabo, ameeleza kuwa serikali imeendelea kuongeza bajeti ya taasisi hiyo kila mwaka kwa lengo la kuboresha miundombinu na mazingira ya kazi.

“Ujenzi wa jengo hili ulianza Januari 27, 2024 na kukamilika Julai 16, 2025 kwa asilimia 100. Ujenzi ulijumuisha jengo kuu, ukuta na miundombinu mingine ya ofisi,” ameeleza.

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeongeza bajeti ya TAKUKURU kwa mafanikio makubwa. Kuanzia bilioni 1.5 mwaka wa fedha 2021/22, bajeti imeongezeka hadi bilioni 6.0 mwaka 2025/26 kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa majengo mapya,ukarabati wa majengo ya zamani pamoja na ujenzi wa uzio kwenye ofisi zisizo na uzio.

Ofisi ya TAKUKURU Kishapu iko katika Mtaa wa Mwasele ‘B’, ndani ya Mamlaka ya Mji Mdogo Kishapu, tofauti na awali ambapo ilikuwa Mtaa wa Makambini katika majengo ya zamani ya Shirecu huku Kauli mbiu ya TAKUKURU ikibaki kuwa: "Kuzuia Rushwa ni Jukumu Lako na Langu Tutimize Wajibu Wetu."

Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala,Katiba na Sheria  na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Boniphace Butondo akizungumza kwenye uzinduzi wa jengo jipya la TAKUKURU Wilayani Kishapu Mkoani  Shinyanga Juni 25,2025 likizinduliwa na Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU Bw.Chrispin Chalamila.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye uzinduzi wa jengo jipya la TAKUKURU Wilayani humo Juni 25,2025 likizinduliwa na Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU Bw.Chrispin Chalamila.

Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Ruswa (TAKUKURU) Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Atuganile Stephen.

Mkazi wa Mtaa wa Mwasele "B" Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Amos Masunga akizungumzia umuhimu wa uwepo wa ofisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kupiga vita uwepo wa Rushwa kwenye jamii hiyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson.

Matangazo

  • TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA KWA KIPINDI KILICHOISHIA TAREHE 30 JUNE. 2022 August 14, 2023
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI November 03, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili September 20, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • VIJIJI 16 VINAVYOZUNGUKA MIGODI KISHAPU MIGOGORO YA ARDHI KUKOMESHWA

    June 27, 2025
  • TAKUKURU YAZINDUA JENGO JIPYA KISHAPU, LAWAPA WANANCHI IMANI NA UJASIRI KUPINGA RUSHWA

    June 26, 2025
  • DED KISHAPU AHIMIZA USHIRIKIANO KATI YA NGO's NA SERIKALI

    June 23, 2025
  • TIP YAENDESHA MAFUNZO YA KUPINGA UKATILI KISHAPU

    June 17, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa