Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoani Shinyanga limetoa msaada wa mashuka na sabuni za kufulia kwa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Kishapu – Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Meneja wa TANESCO Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhandisi Hussein Mbulu akizungumza walipokuwa wakikabidhi msaada wa mashuka na sabuni za kufuria kwenye Wodi ya wazazi wanapoendelea na maadhimisho ya Wiki ya huduma kwa wateja Hospitali ya Dr.Jakaya Mrisho Kikwete Wilayani humo Oktoba 7,2025
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kishapu akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo Oktoba 7,2025 Mhandisi Hussein Mbulu, amesema msaada huo ni ishara ya kujali wateja na jamii, sambamba na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu, Dkt. Charles Mlonganile akizungumza baada ya kupokea msaada huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoani Shinyanga Oktoba 7,2025
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Charles Mlonganile, ameishukuru TANESCO kwa mchango huo na kuwataka wadau wengine kuendelea kushirikiana na serikali kuboresha huduma za afya wilayani Kishapu.






Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa