• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utawala
      • Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya jamii
      • Afya
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Tehama
      • Utamaduni, Sanaa na Michezo
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Usafi wa Mazingira na Udhibiti Taka
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Kilimo na Mifugo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya picha na video za shughuli za maendeleo

TIP YAFANYA MAFUNZO REJEA DHIDI YA UKATILI KISHAPU

Posted on: September 3rd, 2025

Mratibu Mwandamizi Kutoka TIP Livinus Ndibalema akizungumza kwenye kikao cha mafunzo rejea kuhusiana na kutokomeza masuala ya ukatili wa Wanawake na Wasichana hasa wenye ulemavu kikao kilichowakutanisha Viongozi wa Dini,Walimu na viongozi wa Mila Septemba 3,2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga

Katika mwendelezo wa jitihada za kuhakikisha jamii ya Kishapu Mkoani Shinyanga inakuwa salama kwa Wanawake na Watoto hasa wenye ulemavu, Muungano wa Taasisi za Kidini Tanzania (TIP) unaotekeleza mradi wa "Chaguo Langu Haki Yangu" umefanya mafunzo rejea kwa Viongozi wa Dini, Waalimu wa Madrasa, Shule za Jumapili na Viongozi wa Kimila kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo.


Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo mnamo Septemba 3,2025 yakilenga kukumbusha na kupima hatua zilizofikiwa tangu mafunzo ya awali, hususani katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, ndoa za utotoni, ukeketaji na mila kandamizi zinazowanyima Wanawake na Watoto wa Kike nafasi ya kuishi kwa furaha na heshima.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo na Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Kishapu Bernadetha Bagenzi amesema zoezi hilo la mafunzo rejea limekuwa chachu ya tathmini ya utekelezaji wa majukumu yaliyokabidhiwa kwa washiriki kwenye jamii zao.

“Ni muhimu kufuatilia kwa vitendo yale tuliyojifunza, ili tuone kama kweli elimu inayotolewa inaleta mabadiliko katika maisha ya watu,” amesema Bagenzi.

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga na mwakilishi kutoka serikalini Abednego Madole akizungumza kwenye kikao cha mafunzo rejea Kilichoratibiwa na Shirika la TIP na kuwakutanisha Viongozi wa Dini,Walimu na viongozi wa Mila kuhusu ukatili wa kijinsia Septemba 3,,2025 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo

Serikali Yapongeza Ushirikiano
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kishapu, Abednego Madole, amelipongeza Shirika la TIP kwa kushirikiana na Serikali katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia, hasa kwa Wanawake na Wasichana wenye ulemavu.

Madole ameongeza kuwa Viongozi wa dini wana nafasi ya kipekee kwa sababu husikilizwa na jamii. Ni wajibu wao kutumia mimbari zeo kuelimisha juu ya haki za watu wenye ulemavu, kuondoa dhana potofu za kuwaficha watoto wenye ulemavu, na kuhimiza uboreshaji wa miundombinu rafiki katika nyumba za ibaada za wenye ulemavu pia.

"Watumishi wa Mungu na Viongozi wetu elimu yenu itasaidia kupunguza mauaji katika ndoa na kuimarisha mshikamano wa kifamilia,waelemisheni wafahamu ni wapi wanapaswa kupeleka mashitaka pindi wanapofanyiwa ukatili wowote” amesema Madole.

Ameongeza kuwa Walimu wa Madrasa na Shule za Jumapili wana jukumu kubwa la kuwa chachu ya mabadiliko, kwa kuwajengea watoto msingi wa kimaadili na kuwalea wawe watu wazima bora na wenye maono chanya.

                               Jamii Yaonyesha Mabadiliko

Washiriki wa mafunzo kwa pamoja wamebainisha kuwa jamii ya Kishapu sasa imeanza kuonyesha mwamko mkubwa wa kuachana na mila na desturi zisizo na tija kwa Wanawake na Watoto wa Kike. 

Wamesema kuwa ndoa na mimba za utotoni zimeanza kupungua, huku wananchi wakionyesha utayari wa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kwa vyombo husika vya kisheria.

“Jamii sasa imeanza kuelewa kuwa kumlinda Mtoto wa kike ni kulinda taifa zima. Kuna mabadiliko makubwa yanayoonekana, na sisi viongozi tumejipanga kuyaendeleza,” wamesema washiriki kwa kauli ya pamoja.

 Kupitia mafunzo hayo, Mratibu Mwandaizi wa miradi kutoka TIP Livinus Ndibalema amesema TIP imeendelea na itaendelea kujenga mshikamano kati ya Viongozi wa Dini, Serikali na wadau wengine wa maendeleo ili kuhakikisha vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia vinakomeshwa kabisa na wote wapate haki sawa za maamuzi.

Aidha washiriki wameweka mipango ya pamoja watakayotekeleza katika kipindi hiki cha kumalaizia mwaka watatu wa utekelezaji mradi wa "Chaguo Langu Haki yangu" ikiwa ni pamoja na kutoa semina za pamoja za mara kwa mara kwa waalimu wengine wa dini,kutoa eimu mashuleni wakati wa vipindi vya dini kupitia (mpango wa Shule salama), kutoa elimu kwenye vikundi mbalimbali vya (watoto,wanawake na vijana) na kutoa elimu kupitia mikusanyiko mbalimbali kwenye jamii.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI December 22, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 21, 2025
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • RC MHITA AWATAKA MADIWANI KISHAPU KUDUMISHA USHIRIKIANO NA MSHIKAMANO - NGUZO KUFANIKISHA MIPANGO YA MAENDELEO.

    December 19, 2025
  • DED JOHNSON ATOA MAELEKEZO MUHIMU KWA MADEREVA

    December 19, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WAMTEUA MWENYEKITI MPYA HALMASHAURI YA WILAYA KISHAPU

    December 03, 2025
  • WATUMISHI KISHAPU WAPEWA MAFUNZO YA ELIMU YA FEDHA NA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI

    November 20, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa