VIJANA 648 JIMBO LA KISHAPU WAANZA MAFUNZO YA SIKU 2 KWAAJILI YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.

Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga wameanza mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wasaidizi na Waendeshaji wa vifaa vya Bayometriki wapatao 648 watakaosambazwa kwenye Vituo 324 kwa ajili ya kazi ya uboreshaji wa taarifa katika Daftari la kudumu la wapiga kura .

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo yanayoendelea katika kumbi tofauti tofauti katika Jimbo la Kishapu, Afisa Mwandikishaji wa Jimbo Kishapu Ndugu, Emmanuel Johnson ametoa wito kwa Wananchi wote wenye sifa za kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura litakalo anza Tarehe 21-27 Agosti 2024 kufika katika vituo vilivyo kwenye maeneo yao ili waweze kuboresha taarifa zao,

Aidha Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kishapu ametumia furusa hiyo kuwapongeza washiriki wote kwa kuteuliwa na Tume kuendesha na kusimamia zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura.

“Sina shaka kuwa kuteuliwa kwenu kunatokana na ujuzi,uwezo na weledi mlionao katika kutekeleza majukumu ya kitaifa likiwemo zoezi la uboreshaji wa Daftari ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025”Amesisitiza Afisa Mwandikishaji Jimbo la Kishapu Ndugu, Emmanuel Johnson.
@tumeyauchaguzi_tanzania

Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa